Waziri Ummy azindua Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kwa watumishi wa afya kuhusu ugonjwa wa Uviko - 19
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Donald Wright, Mkurugenzi wa Shirika la kudhibiti na kukinga magojwa (US Centers for Disease Centrol and Prevention - CDC), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa Afya (Extension of Community Health and Care Outreach – ECHO) leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Kituo hicho kimeanzishwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la CDC. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wataalam wa afya wanaoendesha kituo cha mafunzo kwa njia ya mtandao kuhusu ugonjwa wa Uviko – 19 kwa watumishi wa afya wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la kudhibiti na kukinga magojwa ya (US Centers ...