Serikali yanunua mashine za kisasa za ECHO zinazotumika katika Hospitali za Kanda na Rufaa
Mtaalam kutoka kampuni ya General Electric (GE) Judith
Nyamboga akiwapa maelekezo madaktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI), hospitali za Kanda Mbeya, KCMC, Bugando, Benjamini Mkapa na hospitali
za Rufaa Mtwara na Chato namna ya kutumia mashine ya Echocardiogram – ECHO inazotumika
kuchunguza jinsi moyo unavyofanya kazi wakati wa mafunzo ya siku tatu
yaliyofanyika JKCI kwa madaktari hao baada ya mashine za kisasa za ECHO
kununuliwa na Serikali na kupelekwa katika hospitali hizo kwaajili ya kutoa
huduma kwa wagonjwa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Henry Mayala akiwaongoza madaktari wenzake kutoka hospitali za
Kanda Mbeya, KCMC, Bugando, Benjamini Mkapa na Hospitali za Rufaa Mtwara na
Chato kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kutumia
mashine ya Echocardiogram – ECHO wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika
katika Taasisi hiyo kwa madaktari hao baada ya Serikali kununua mashine za
kisasa za ECHO ambazo zimepelekwa katika hospitali hizo kwaajili ya kutoa
huduma kwa wagonjwa.
Picha na: Genofeva Matemu
***************************************************************************************
Comments
Post a Comment