Tumieni maonesho ya Sabasaba kupima magonjwa ya Moyo
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zenais Ngowi
akiwaelezea wananchi namna ambavyo mashine ya kusaidia kupumua (ventilator)
inavyotumika kwa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU)
wakati wa maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya
Kilwa.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maklina
Komba akimfanyia usajili mwananchi aliyefika katika banda la JKCI lililopo
katika maonesho ya Sababasa Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za
vipimo vya magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Anastazia Moshi akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyetembelea banda
la JKCI leo lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
vilivyopo katika barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata
huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Mteknolojia wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Jordan Megabe akimwambia namna vipimo alivyoandikiwa na daktari
vitakavyofanyika katika maabara mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo
kwa ajili ya kupimwa vipimo vya magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa maonesho
ya 46 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro
Pallangyo akimsikiliza mwananchi aliyefika katika banda hilo kwa ajili ya
kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa maonesho ya 46 ya
Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.
*****************************************************************************************************
Wananchi wajitokeza kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo na
kisukari katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na kuvutiwa na huduma
zinazotolewa.
Uchunguzi huo unafanyika katika Banda la Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete lililopo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza alipotembelea banda la JKCI Mkazi wa Kisutu
Jijini Dar es Salaam Mama Shainul Fernandis alisema kuwa amefika katika banda la
JKCI na kupata fursa ya kuulizwa maswali kuangalia elimu aliyonayo kuhusu
magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na moyo magwojwa ambayo kwa kiingereza
wanaita silent killer hivyo baada ya kuangalia uwelewa wake na kupata nafasi ya
kupima sukari mwilini, shinikizo la damu na vipimo vya moyo.
“Nashukuru baada ya vipimo nimepata ushauri wa kuwa napima
sukari yangu mara kwa mara kwani wameona sukari yangu imeanza kuwa juu, pia
watoa huduma niliowakuta katika banda la JKCI walikua wavumilivu kutusikiliza
na kutusaidia jambo ambalo linatoa motisha kwetu kuwa huru kujieleza kwa
uhuru”,
“Sabasaba mbali na watu kuja kutembea, kuona wanyama na
kufanya manunuzi ya vitu ni vyema pia kutembelea mabanda haya yanayotoa huduma
za kuchunguza afya ili kujua afya zetu, Sikutegemea kama nikija kwenye maonesho
haya nitapata nafasi hii ya kuchunguza afya yangu”, alisema Mama Shainul
Aidha Mama Shainul alitoa wito kwa wananchi kuwa na tabia ya
kuchunguza afya mara kwa mara kwani mazoea ya kusubiri hadi kuumwa ndio mtu
achunguze afya yake huwaza kusababisha gharama za kulitatua tatizo hilo kuwa
kubwa zaidi tofauti na kama matibabu yangefanyika wakati wa awali kabla ya
tatizo kuwa kubwa.
Naye mkazi wa Gongo la Mboto Salehe Kipanga alisema kuwa
baada ya Kutembelea banda la JKCI na kufanyiwa uchunguzi aligundulika kuwa na
tatizo la sukari na shinikizo la damu hivyo kuhamashishwa kufanya na vipimo vya
moyo ambavyo kwa hapo Sabasaba vinafanyika kwa bei nafuu.
“kwa kweli Taasisi hii inayojishughulisha na utoaji wa huduma
za matibabu ya moyo inahitaji pongezi, wametufanyia vipimo vya moyo kwa bei
nafuu sana tofauti na kama ningeenda katika hospitali zinazotoa huduma hii.
Shinikizo langu la damu halikuwa vizuri sana lakini daktari
kanishauri nisitumie dawa kwanza bali nifuatilie ikiwezekana kila siku kwa
kupima hadi hapo itakapoonekana nahitaji kutumia dawa ndio nitumie dawa, kwa
upande wa sukari mwilini nimepatiwa dawa
ambazo nitaenda kuzitumia na kufuatilia muenendo wa sukari mwilini kwani kwa
kufanya hivyo nitaweza kuepuka athari zinazotokana na magonjwa haya.
Abdalla Sidick Mkazi wa Temeke Anasema kuwa hii ni mara yake
ya kwanza kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo toka kuzaliwa kwake jambo
ambalo hakuwahi kufikiria kama angefanya.
“Sasa nina miaka 42 na leo nimepata fursa hii ya kuujua moyo
wangu, nimefurahi sana kukuta niko salama na elimu niliyoipata hapa nitaifanyia
kazi ili moyo wangu uendelee kuwa salama siku zote kwani magonjwa haya yasiyo ambukiza
ni hatari”,
“Wito wangu kwa vijana ambao umri umeanza kusogea ni vizuri
tukachunguza afya zetu, tukabadili mifumo yetu ya maisha ili tunapoelekea
kwenye umri wa utu uzima tusipate changamoto za magonjwa yasiyoambukiza kama
ugonjwa wa moyo na kuzipa gharama familia zetu kwani magonjwa haya yanahitaji
fedha nyingi kuyatibu”, alisema Sidick
Comments
Post a Comment