Wajumbe kutoka Bohari ya Dawa Msumbiji (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) ya nchi hiyo watembelea JKCI kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tulizo Shemu akiwaeleza wajumbe kutoka Bohari ya Dawa Msumbiji (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) jinsi huduma za matibabu ya moyo zinavyotolewa katika Taasisi hiyo wakati wajumbe hao walipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah
Kimambo akizungumza na ujumbe kutoka
Bohari ya Dawa Msumbiji (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) ya
nchini humo walipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa. Kushoto ni Mfamasia
kutoka Bohari ya Dawa (MSD) Faith Edwin.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo na ujumbe kutoka Bohari ya Dawa Msumbiji (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) ya nchini humo mara baada ya kumaliza ziara yao leo ya kutembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na Khamisi Miharo
Comments
Post a Comment