WANANCHI 761 WAPATA HUDUMA YA TIBA MKOBA YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumalizika kwa mbio za Siha Marathon 2023 zilizofanyika hivi karibuni mkoani Kilimanjaro. Wananchi wa Siha wakijadili mambo mbalimbali huku wakisubiri kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku sita ya upimaji na matibabu ya moyo iliyomalizika hivi karibuni katika hospitali ya Wilaya ya Siha. Na: JKCI ********************************************************************************************** Watu 761 wamepata huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya moyo katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Wilaya Siha. Kambi hiyo ilifanyika kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 18 hadi 23/12/2023 ambapo watu w...