Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo wilayani Siha


Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe bora kwa wananchi waliofika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

*************************************************************************************************************************************
************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospiitali ya Wilaya ya Siha iliyopo mkoani Kilimanjaro watatoa huduma za tiba mkoba ijulikanayo kwa  jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Wilaya ya Siha na Wilaya jirani.

Upimaji huu ambao utaenda sambamba na ushiriki wa JKCI katika mbio za Siha Marathon utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 18/12/2023 hadi tarehe 22/12/2023  saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Viwanja  vya Hospitali ya Wilaya Siha.

Kutakuwa na madaktari bingwa  wa moyo watakaoambatana na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanayoweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

 

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0713164432 Dkt. Haji Mnasi Mkurugenzi wa Wilaya Siha, 0789113311 Dkt. Paschael Mbota Mganga Mkuu wa Wilaya Siha na 0755402718 Dkt. Nsubili Mwakapege  Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Siha.

                       

 “Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari