Kwa mara ya kwanza Valvu ya moyo yabadilishwa bila kufanya upasuaji wa kufungua kifua


Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India wakifanya upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI) katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayofanyika JKCI. Upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumfanyia mgonjwa upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI) katika kambi maalumu ya siku mbili ya matibabu ya moyo inayofanyika JKCI. Upasuaji huo mdogo wa kubadilisha valvu umefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo