Siha wajitokeza kwa wingi kupima moyo
Daktari bingwa wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Ludovick akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Christopher Timbuka namna kipimo cha kuangali jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO) kinavyofanyika wakati alipotembelea kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Siha.
Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Christopher Timbuka akimsikiliza Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mainda Hamis wakati alipotembelea kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo inayofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Siha.
Daktari bingwa wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Ludovick akiwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali ya Wilaya ya Siha namna ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo ya siku tano inayofanyika katika Hospitali hiyo. Pamoja na kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wanannchi JKCI pia inawajengea uwezo wa jinsi ya kutibu na kuwatambua wagonjwa wa moyo wataalamu wa afya wa Hospitali ya Wilaya hiyo
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akimpa elimu ya lishe bora Mama Holdersifa Swai ambaye alifanyiwa upasuaji mkubwa wa kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Bypass Graft Surgery - CABG) mwaka 2021 katika Taasisi hiyo aliyefika katika kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Siha.
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo.
Comments
Post a Comment