Dkt. Mollel: Wataalamu wa Afya tengeni muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wacheza ngoma ya kimaasai wakati wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea shamba la wanyamapori Serval Wildlife kwaajili ya kufanya utalii wa ndani. Wataalamu wa JKCI walikuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo.
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Taasisisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea shamba la wanyamapori Serval Wildlife kwaajili ya kufanya utalii wa ndani. Wataalamu wa JKCI walikuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo.
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakicheza ngoma ya kimaasai walipotembelea Osiligilai Maasai Lodge kwaajili ya kufanya utalii wa ndani. Wataalamu wa JKCI walikuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo.
*********************************************************************************************************************************************************************************************************************
Wataalamu wa afya nchini wametakiwa kipindi wanachokuwa likizo kutenga muda wa kufanya utalii wa ndani ili kujionea vivutio mbambalimbali vilivyopo kwa kufanya hivyo kutasaidia kupumzisha akili zao.
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Afya na
Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel wakati akiongea na waandishi wa
habari kuhusu utalii tiba unavyoendana na utalii wa vivutio mbalimbali
vilivyopo nchini.
Mhe. Dkt. Mollel ambaye aliambatana na wataalamu wa Taasisisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutembelea shamba la
wanyamapori Serval Wildlife lililopo
wilayani Siha kwaajili ya kufanya utalii wa ndani.
Alisema wataalamu wa afya wanafanya kazi kubwa na ngumu ya
kuokoa maisha ya wagonjwa hivyo basi ni muhimu kipindi wanapokuwa likizo wakatenga
muda wa kupumzisha akili zao kwa kutembellea vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyopo nchini kwa kufanya hivyo wataweza kufanya kazi zao vizuri zaidi kwani
ukiwa na akili iliyotulia utaweza kufanya kazi ngumu kirahisi.
“Leo nimekuja hapa kuwapa zawadi wataalamu wa JKCI waliyopewa
na Mhe.Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, zawadi hii tumewapa baada ya Mhe. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan kuimarisha miundombinu ya afya alisema tuanze kufanya
utalii tiba na taasisi ya kwanza kuelewa hili jambo na kuanza kulitekeleza ni
JKCI na wengine wakafuata”,.
“Nimekuja hapa kuwaonesha jinsi utalii tiba unavyoendana na
utalii wa kawaida wameona utalii uliopo kwa kujua kwao kutasaidia kuwajulisha
wagonjwa kutoka nje ya nchi wanaowatibu kuwahamasisha kutembelea vivutio
vilivyopo pindi watakapoona”, alisisitiza Mhe.Dkt. Mollel.
Kwa upande wake Fawad Hamoud Mkurugenzi Mtendaji wa shamba la
wanyamapori Serval Wildlife aliwashukuru
wataalamu wa JKCI kwa kutembelea shamba hilo na kusema kuwa JKCI imekuwa ni taasisi ya kwanza kutembelea mahali hapo na
kupata nafasi ya kulisha wanyama na kupiga nao picha.
Fawad alisema katika shamba hilo wanajishughulisha na ufugaji
wa wanyamapori wambao ni tofauti na ufugaji wa wanyama wengine walioko Zoo kwani
ukiwa katika shamba hilo unakaa karibu na Wanyama akiwemo simba unawalisha
chakula na kupiga nao picha.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutupa nafasi ya kufanya uwekezaji
mahali hapa na tunatumia nafasi hii kutangaza utalii , tunapokea wageni wengi
kutoka ndani na nje ya nchi kuja kuona wanyama tunawaomba wananchi mje mahali
hapa kulisha wanyama na kupiga nao picha”, alisema Fawad.
Nao wafanyakazi wa JKCI waliotembelea vivutio hivyo
walimshukuru Waziri wa Afya kwa kuwapa nafasi hiyo na kusema kuwa wameona utalii
uliopo na hiyo itawasaidia kutangaza vivutio hivyo kwa wagonjwa wanaowatibu pamoja
na wataalamu wa afya wanaokuja kufanya kambi za upasuaji wa moyo kutoka nje ya
nchi.
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walikuwa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa huduma za upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi na kutumia nafasi hiyo kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika wilaya hiyo.
Comments
Post a Comment