Posts

Showing posts from May, 2025

JKCI kuwafanyia uchunguzi wa moyo wateja wa ATC

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mashirikiano kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na viongozi kutoka Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) wakati wa kikao cha kuangalia namna ambavyo watashirikiana kutoa huduma kwa wateja wanaotumia shirika hilo kupata huduma za uchunguzi wa afya katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).  Meneja masoko wa Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL) Christina Tungalaza akifafanua jambo wakati wa kikao cha kujadili namna shirika hilo linaenda kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za uchunguzi wa afya kwa wateja wake jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akisalimiana na viongozi kutoka ...

Wafanyakazi wa JKCI watakiwa kufanya kazi kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma

Image
Katibu wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aliyemaliza muda wake  Abdulrahman Muya  akimkabidhi nyaraka za utendaji kazi Katibu mpya wa baraza hizo Adam Sembe aliyechaguliwa katika katika  mkutano wa tatu wa baraza jipya la wafanyakazi wa Taasisi hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule akizungumza na wajumbe wa baraza jipya la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule zawadi kutoka kwa taasisi hiyo mara baada ya kufungua mkutano wa tatu wa baraza jipya la wafanyakazi wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Baadhi wa wajumbe wa  baraza jipya la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiimba wimbo wa “solidarity forever” wakati wa ufunguzi...

Wauguzi 11 wahitimu mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Prof. Neema Mori wa    Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kozi ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yaliyotolewa na JKCI kwa kushirikiana na UDSM. Hafla fupi ya kumaliza mafunzo hayo ilifanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa JKCI jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.Peter Kisenge akimkabidhi Afisa Muuguzi kutoka hospitali ya Jeshi Mwanza    Juma Sagida cheti cha kuhitimu mafunzo     ya kuwahudumia watoto mahututi katika hafla fupi     ya kumaliza kozi hiyo iliyofanyika jana jijini     Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Moyo Zambia Misozi Sibande cheti cha kuhitimu mafunzo   ya kuwahudumia watoto mahututi na kutoa huduma za Cathla...

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu  ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mshauri wa Rais wa Burkina Faso na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Afya wa Rais, Drissa Traore wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma bobezi za matibabu ya moyo mara baada ya kuisaini jana jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pe...

JKCI kuwa kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto Afrika Mashariki na Kati

Image
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Che Mingjian, wakibadilishana  Mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete eneo la Mloganzila kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto Afrika Mashariki na Katipamoja na mradi wa ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu, hafla iliyofanyika jijini Dodoma. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Che Mingjian, wakitia saini Mikataba miwili ya msaada wa jumla ya Yuan za China milioni 500, sawa na shilingi bilioni 185 kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete enelo la Mloganzila kuwa Kituo cha Umahiri cha matibabu ya moyo kwa watoto  Afrika Mashariki na Kati  pamoja na mradi wa ushirikiano wa kiuchumi n...

Watoto 39 wafanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu

Image
  Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)   na wanzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kuziba tundu la moyo mtoto wakati wa kambi maalumu ya siku tano iliyomalizaka jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 39 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na upasuaji wa tundu dogo. Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka nchini Cameron kupitia Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimalizia kumfunga kifua mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano iliyomalizaka jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 39 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na upasuaji wa tundu dogo. Na: JKCI *************************************************************************************************************************** Watoto 39 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefany...

Wataalamu kutoka Shirika la Mending Kids International wapongezwa kwa kushirikiana na JKCI kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto 39

Image
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Shirika la Mending Kids International la nchini Marekani baada ya kumalizika kwa kambi maalumu ya siku tano ya upasuaji wa moyo kwa watoto 39. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akimpatia zawadi daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka Shirika la Mending Kids International la nchini Marekani Sasha Agati baada ya kumalizika kwa kambi maalumu ya siku tano ya upasuaji wa moyo kwa watoto.  Watoto 39 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akimpatia zawadi mratibu kutoka Shirika la Mending Kids International la nchini Marekani Dulcie Morris baada ya kumalizika kwa kambi maalumu ya siku tano ya upasuaji wa moyo kwa watoto.  Watoto 39 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa...

JKCI na Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la Italia wasaini mkataba wa kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo Afrika

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge  na Rais wa Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la nchini Italia Palumbo Vincenzo wakibadilishana mkataba wa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo  barani Afrika wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Rais wa Shirika la UNA VOCE PER PADRE PIO la nchini Italia Palumbo Vincenzo wakionesha mkataba wa kuwatibu watoto wenye matatizo  ya moyo waliopo barani Afrika wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. ************************************************************************************************************************************************************************************************************************* Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)...

GSM Foundation na Yanga wachangia milioni 50 za matibabu ya moyo kwa watoto

Image
Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 fedha zilizotolewa na GSM Foundation na klabu hiyo kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea taasisi hiyo leo kwa ajili ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 50 fedha zilizotolewa  na GSM Foundation na klabu hiyo kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza Rais wa klabu ya mpira ya Yanga Eng. Hersi Said alipotembelea taasisi hiyo leo kwa ajili ya kukabidhi hundi ya shilingi...

Zanzibar waendelea kupata huduma za matibabu ya moyo

Image
Wakazi wa Zanzibar wakiwa katika foleni ya kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport. Wakazi wa Zanzibar wakipata huduma mbalimbali katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport Zanzibar. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akiwafundisha wanafunzi namna huduma za matibabu ya moyo zinavyofanyika wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika viwanja vya Golden Tulip Airport. Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Heart Team Africa Foundation (HTAF) Linda Gideon akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Zanzibar mara baada ya kuchangia matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto kwa kununua T-shirt wakati wa maonesho ya wiki ya Afya Zanzibar yanayoendelea katika v...