JKCI kuwahudumia wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah wakionesha hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) mara baada ya kusaini mkataba huo leo katika hoteli ya protea iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) leo katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah, wafanyakazi wa AU na JKCI wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) leo katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah wakibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) leo mara baada ya kusaini hati hiyo katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Huduma za tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wafanyakazi wa Umoja wa Afrika (AU) leo katika Hoteli ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam.

Na JKCI

**************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Umoja wa Afrika (AU) Kurugenzi ya Huduma za matibabu na afya wamesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma za matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo kwa wafanyakazi wa umoja huo.

Hati hiyo ya makubaliano imesainiwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Umoja wa Afrika Dkt. Adamu Isah mara baada ya AU kuridhishwa na ubora wa huduma, wataalamu wa JKCI na uwekezaji wa vifaa tiba vya kisasa vilivyopo katika Taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge alisema ushirikiano huo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika vifaa tiba na rasilimali watu hivyo kuiwezesha taasisi hiyo kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi.

“Leo JKCI imeandika tena historia nyingine nchini ya kusaini makubaliano na Umoja wa Afrika katika kuwahudumia wafanyakazi wa AU ambao watapata changamoto za kiafya kwa kuwa na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo”, alisema Dkt. Kisenge

Dkt. Kisenge ameongeza kuwa makubaliano hayo yanaonesha namna uwekezaji katika wataalamu na teknolojia za kisasa za tiba unavyoweza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuongeza imani ya taasisi za kimataifa kutaka kupata huduma nchini Tanzania.

“Taasisi inawahudumia wananchi kutoka nchi zaidi ya ishirini ambazo zinakuja JKCI kupata huduma za matibabu ya moyo na upasuaji, nia ya JKCI ni kuhakikisha kwamba inatoa huduma za matibabu ya moyo zenye ubora wa juu”, alisema Dkt. Kisenge.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Umoja wa Afrika (AU) Dkt. Adamu Isah alisema AU imeamua kuingia makubaliano na JKCI baada ya kufanya tathmini ya huduma zinazotolewa na kuridhishwa na utaalamu wa madaktari, uwezo wa uchunguzi na vifaa tiba vilivyopo katika taasisi hiyo.

“Tulikuja hapa mwaka mmoja uliopita na tumeona ubora wa huduma kutoka kwa wataalamu, wana uwezo wa kufanya uchunguzi na matibabu ya kibingwa ya moyo, tumejiridhisha na kuona wamekidhi viwango tunavyohitaji kwa ajili ya kuwahudumia wafanyakazi wa AU hivyo tumekubaliana kushirikiana na taasisi hii na tunafurahi kusaini mkataba huu leo”, alisema Dkt. Isah.

Makubaliano hayo yanaongeza fursa ya JKCI kuendelea kutumia utaalamu na miundombinu yake kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika huku yakiimarisha ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Afrika (AU) katika sekta ya afya.




Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma