JKCI na TPDC waweka kambi ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali
ya Dar Group Marsia Tillya akimsikiliza mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika
kambi maalumu ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kuelekea mbio za TPDC
zitakazofanyika tarehe 21 mwezi Novemba mwaka huu kwaajili ya kuchangia
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Flora Anderson akimpima shinikizo la damu mkazi wa Dar es Salaam wakati wa kambi maalumu ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kuelekea mbio za TPDC zitakazofanyika tarehe 21 mwezi Novemba mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Monica
Elias akimpima shinikizo la damu Jackline Mhando wakati wa kambi maalumu ya
uchunguzi wa magonjwa ya moyo kuelekea mbio za TPDC zitakazofanyika tarehe 21 mwezi
Novemba mwaka huu kwaajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya
moyo wanaotibiwa na JKCI.
Na JKCI
**************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwakushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
wameweka kambi maalumu ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa
Dar es salaam kurahisisha upatikanaji wa huduma bingwa bobezi karibu na
wananchi.
Kambi hiyo maalumu inafanyika
kwa siku tatu ikiwa ni sehemu za harakati za kuelekea mbio za TPDC marathon
zinazotarajiwa kufanyika tarehe 21 mwezi Novemba mwaka huu kuchangia gharama za
matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na JKCI.
Akizungumza wakati wa kambi
hiyo daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) hospitali ya Dar Group Marsia Tillya alisema wananchi wa Dar es Salaam
pamoja na washiriki wa mbio za TPDC mwaka huu wanatakiwa kutumia fursa hiyo
kupima afya zao na kujua namba zao muhimu za afya.
“Ni muhimu washiriki wa mbio
za TPDC marathon mwaka 2026 wakafika katika viwanja hivi vya mnazi mmoja na
kupima magonjwa ya moyo bila gharama ili wanapoenda kushiriki mbio hizo wawe na
uhakika wa afya zao”, alisema Dkt. Marsia
Dkt. Marsia alisema wanamichezo
wapaswa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ikiwemo kupima moyo ili waweze
kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa michezo”, alisema Dkt. Marsia
Kwa upande wake Mkazi wa jiji
la Dar es salaam Nicodemus Yohana aliyepata huduma katika kambi hiyo alisema
amefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa na JKCI huku akifurahia zaidi na elimu
ya utambuzi wa dalili za magonjwa yasiyoambukizwa aliyoipata kupitia kambi hiyo.
“Kiukweli ni muhimu sana
kuzingatia afya zetu kwa kupima mara kwa mara, watoa huduma wametupa elimu ya
kutosha kuhusu magonjwa haya ya moyo na dalili zake”, alisema Yohana.
Naye Elizabeth Clemence mkazi
wa Dar es salaam aliiomba Serikali kupitia JKCI kuendelea kuweka kambi za
matibabu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam ili wananchi waweze
kupata mwamko wa kujitokeza na kupima afya zao.
“Natamani kila anayepita
katika viwanja hivi apate mwamko wa kupima afya yake kwani huduma hizi
zinagharama kubwa na wakati mwingine watu hushindwa kuzipata kutokana na sababu
mbalimbali za kimaisha”, alisema Elizabeth.



Comments
Post a Comment