Daktari bingwa wa Moyo kutoka Misri kufanya upasuaji JKCI
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Ghati Chacha akimkaribisha Balozi wa Tanzania Nchini Misri Mhe. Emmanuel
Nchimbi alipowasili katika Taasisi hiyo huku akiongozana na wageni kutoka Taasisi
ya Ushirikiano wa Afrika na Asia (AFASU) iliyopo nchini Misri kwa ajili ya
kujenga mashirikiano katika masuala ya tiba ili kuboresha huduma za afya nchini
hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane akielezea huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati ugeni kutoka Taasisi ya Ushirikiano wa Afrika na Asia (AFASU) iliyopo nchini Misri ulipotembelea JKCI kwa ajili ya kujenga mashirikiano katika masuala ya tiba ili kuboresha huduma za afya nchini hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Ghati Chacha akizungumza na wageni kutoka Taasisi ya Ushirikiano wa Afrika
na Asia (AFASU) iliyopo nchini Misri kwa ajili ya kujenga mashirikiano katika
masuala ya tiba ili kuboresha huduma za afya nchini hivi karibuni
walipotembelea Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) na wageni kutoka Taasisi ya Ushrikiano wa Afrika na Asia (AFASU)
kutoka nchini Misri wakifuatilia taarifa iliyokua ikitolewa wakati wageni hao
walipotembelea JKCI kwa ajili ya kujenga mashirikiano katika masuala ya tiba
ili kuboresha huduma za afya nchini hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo
Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania Nchini Misri Mhe. Emmanuel Nchimbi
akielezea umuhimu wa ujio wa wageni kutoka Taasisi ya Ushirikiano wa Afrika na
Asia (AFASU) kutoka nchini Misri walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) hivi karibuni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujenga mashirikiano
katika masuala ya tiba ili kuboresha huduma za afya nchini.
Balozi wa Tanzania Nchini Misri Mhe. Emmanuel Nchimbi katika
picha ya pamoja na viongozi wa menejimenti ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) na wageni kutoka Taasisi ya Ushrikiano wa Afrika na Asia (AFASU) baada
ya ziara yao JKCI kwa ajili ya kujenga mashirikiano katika masuala ya tiba ili
kuboresha huduma za afya nchini hivi karibuni katika Taasisi hiyo iliyopo
Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Khamis Mussa
**************************************************************************************
Nchi ya Misri kupitia Taasisi ya Ushirikiano wa
Afrika na Asia (AFASU) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Misri
imefanikiwa kumleta daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na upasuaji mdogo wa
moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kubadilishana
ujuzi na kujenga uwezo.
Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni katika Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam Balozi wa Tanzania Nchini Misri
Mhe. Emmanuel Nchimbi alisema kuwa katika mazingira ya ushirikiano baina ya
Tanzania na Misri AFASU wameona ni muhimu kumleta Daktari bingwa wa magonjwa ya
moyo nia ikiwa ni kuendeleza mashirikiano ili kuboresha huduma za afya hapa
nchini.
“Kama Ubalozi wa Tanzania nchini Misri tutaendelea kufanya
jitihada ambazo zitaboresha zaidi eneo la afya ambapo kwa kuanzia leo tupo JKCI
na daktari ambaye ni bingwa katika magonjwa ya moyo ili watanzania wenzetu wawe
na afya bora kwa maendeleo ya nchi yetu”,
“Dkt. Ahmed Rezq ni daktari bingwa na mkufunzi wa vyuo vikuu
vitatu duniani ambaye ameshafanya maelfu ya upasuaji wa moyo atakua katika
Taasisi hii kwa muda wa siku nne akijitolea kuwahudumia wagonjwa wetu hapa
nchini, naamini kwa siku hizi nne wataalam wetu watapata kitu kipya”, alisema
Mhe. Nchimbi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo na daktari bingwa
wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane
alisema kuwa JKCI imebahatika kupata ugeni kutoka nchini Misri ambao kwa pamoja
wanaenda kuangalia ni kwa namna gani wataweza kujenga uwezo pamoja na kusaidia
wagonjwa wanaotibiwa JKCI.
“Ujumbe huu umekuja JKCI kwa mara ya kwanza nia ikiwa ni
kuongeza ushirikiano baina ya yetu na wao, kujenga uwezo wa Taasisi yetu katika
kutibu magonjwa ya moyo na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kutusaidia sisi
na nchi nyingine za Afrika katika kukabiliana na magonjwa ya moyo”,
“JKCI tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 imeshafanya upasuaji
mdogo wa moyo kupitia tundu dogo kwenye paja kwa wagonjwa zaidi ya elfu 7,
ambapo hadi sasa tuna aina za upasuaji zaidi ya 35 tunazofanya. Kupitia ugeni
huu tutaweza kuongeza aina za upasuaji ambazo tunafanya tukiwa na lengo la
kuwasaidia watanzania”, alisema Dkt. Waane
Naye Rais wa Taasisi ya Ushirikiano wa Afrika na Asia (AFASU)
kutoka nchini Misri Dkt. Hossam Darwish
alisema kuwa wameona umuhimu wa kufanya kazi na JKCI kwasababu moja ya malengo
yaliyopo katika Taasisi hiyo ni pamoja na kujali uhai wa binadamu.
“Namshukuru Mhe. Balozi Nchimbi kwa juhudi zake alizozifanya
leo hii kutukutanisha nanyi, Taasisi yetu ya AFASU ilianza rasmi mwaka 1955
ikiwa na lengo la kuleta maendeleo ya binadamu, kumjali binadamu na kuakikisha
anakua na afya njema”,
“Leo tupo hapa JKCI ili kushirikiane kwa pamoja, kushikana
mikono kwa pamoja kuhakikisha uhai wa binadamu unaokolewa. Tumekuja na daktari
bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Misri ambaye atakua nanyi hapa kwa
kipindi cha siku nne kwa ajili ya kubadilishana uzoefu”, alisema
Comments
Post a Comment