Tanzania na Saudi Arabia kufanya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimwelezea Balozi wa Saudi Arabia nchini
Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na
Taasisi hiyo wakati wa ziara yake aliyoifanya leo JKCI kwa ajili ya kuangalia
maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022.
Kambi hiyo ya matibabu itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo
nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Katibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adv. Maulid Kikondo mara baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akizungumza na wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini humo ambao wako katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Mgonjwa ya Moyo kwa watoto ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akimsikiliza daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela (kulia) wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza kesho tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Abdullah Al Sharyan akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo, madaktari wa watoto kutoka nchini humo na viongozi wa JKCI mara baada ya kumaliza ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 03/09/2022. Kambi hiyo maalum itafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia.
Picha na Khamisi Mussa
Comments
Post a Comment