Wakazi wa Arusha na mikoa jirani wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo

Afisa uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus akimpima kipimo cha kuangalia shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambako inafanyika kambi maalum ya siku tano ya  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika jana tarehe 29/09/2022.

Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabella Mkojera akichukuwa taarifa za mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba  akichukuwa taarifa za mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akichukuwa taarifa za mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.


Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akichukuwa taarifa za mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

Afisa uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimsomea matokeo ya vipimo vya kuangalia kiwango cha sukari mwilini na shinikizo la damu (BP) mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo. Katika kuadhimisha siku ya moyo  duniani tarehe 29/09/2022 wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo.

Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal Kondi akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography-ECG) mwananchi aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambako inafanyika kambi maalum ya siku tano ya  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo.


Afisa uuguzi wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) Basilisa Geay akimpima kiwango cha sukari mwilini mwananchi aliyefika katika viwanja vya ALMC ambako inafanyika kambi maalum ya siku tano ya  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo iliyoanza tarehe 26 hadi 30 mwezi huu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika jana tarehe 29/09/2022.


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smitha Bhalia akimpima mgonjwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC.

 Wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC)  wakipata huduma za kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo katika kambi maalum ya matibabu iliyoanza tarehe 26 hadi 30 mwezi huu. Kambi hiyo inafanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika jana tarehe 29/09/2022.

Wafanyakazi wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wakimuhudumia wananchi aliyefika katika viwanja vya ALMC ambako inafanyika kambi maalum ya siku tano ya  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo iliyoanza tarehe 26 hadi 30 mwezi huu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika jana tarehe 29/09/2022.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa