Prof. Janabi: Matumizi makubwa ya chumvi ni hatari kwa afya ya moyo


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya moyo duniani leo tarehe 29/09/2022. Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitazama kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography) ambacho alipimwa mwananchi aliyefika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya moyo. Katika kuadhimisha siku ya moyo duniani leo tarehe 29/09/2022 wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitazama jinsi mwananchi anavyopimwa kipimo cha kuangalia shinikizo la damu (BP) wakati wa zoezi la siku tano la uchunguzi na matibabu ya moyo linalofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani tarehe 29/09/2022.


Wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika Arusha Lutheran Medical Centre(ALMC)  kwa ajili ya uchunguzi na matibabu ya moyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi awakati akitoa elimu kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka katika maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wakazi wa Arusha kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya kuyaepuka wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022 katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC). 

Daktari  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bridget Ndumbaro akiangalia mishipa ya damu ya mguu wa mwananchi aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022.

Afisa muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus akimpima kipimo cha kuangali mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography-ECG) mwananchi aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambako inafanyika kambi maalum ya siku tano ya  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022.


Afisa muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima kipimo cha kuangalia kiwango cha sukari mwilini mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea kuhusu umuhimu wa watoto wenye matatizo ya moyo kufanyiwa upasuaji mapema wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC).

Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) Elisha Twisa akimkabidhi zawadi  ya shukurani Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika leo tarehe 29/09/2022 katika viwanja vya ALMC. Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani. 

********************************************************************************************************************************************************************

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amewataka wananchi hususani wa mkoa wa Arusha kuacha matumizi makubwa ya chumvi inayosababisha shinikizo la juu la damu ambalo moja ya madhara yake ni kutanuka kwa moyo.

 Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ametoa wito huo leo tarehe 29/09/2022 wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Arusha Lutheran Medica Centre.

 Alisema watu wengi wanapenda kutumia chumvi nyingi katika chakula hasa chumvi mbichi ambayo inaongezwa baada ya chakula kuiva, unywaji wa juisi za kusindika au kuongeza sukari pindi wanapotengeneza juice pamoja na kula kwa wingi vyakula vyenye wanga  vitu ambavyo ni hatari kwa afya ya moyo.

 Mkurugenzi huyo mtendaji alisema ukanda wa Arusha unawafugaji wengi na nyama inapatikana kirahisi kutokana na hali hii watu wengi wanapenda kula nyama choma ambayo asilimia kubwa ya chumvi inayotumika ni mbichi kitu ambacho kitasababisha changamoto ya afya kwa siku za usoni.

 “Magonjwa ya kisukari na Shinikizo la damu yanatokana na mtindo wetu wa maisha hivyo tupunguze sana ulaji wa chumvi na matumizi makubwa ya sukari kwani asilimia 32 ya vifo vinatokana  na magonjwa yasioambukiza hususani moyo na matibabu yake ni gharama kubwa”,.

 “Ili kukabiliana na magonjwa ya moyo wananchi tujitahidi kufuata mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kuacha uvutaji wa sigara, kuacha unywaji wa pombe uliokithiri, kufanya mazoezi ikiwa ni pamoja na kutembea hatua elfu 10 kwa siku  pamoja na kula vyakula  bora”, alisema Prof. Janabi.

 Aidha Prof. Janabi aliwataka wananchi kukata bima za Afya kwani gharama za matibabu zimekuwa zikiongezeka kadri siku zinavyokwenda lakini kama mtu atakuwa na bima ya afya itamsaidia kulipia gharama za matibabu pindi atakapoumwa.

 Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) Elisha Twisa aliwashukuru wataalamu ya JKCI ambao wako katika hospitali hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.

 “Tunawashukuru wenzetu wa JKCI ambao wametuletea huduma za kibingwa za matibabu ya magonjwa ya moyo katika mkoa wetu wa Arusha, tutazidi kushirikiana nao ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii mara kwa mara”, alisema Twisa.

 Mkurugenzi huyo mtendaji wa ALMC alisema hospital hiyo ipo mbioni kuanzisha kitengo cha matibabu ya moyo ili kuwasaidia wananchi waweze kupata huduma hiyo karibu zaidi.

 Mmoja wa wananchi aliyepata huduma za upimaji na matibabu Kulwa Mayombi alisema yeye pamoja na wenzake wamefurahia kupata huduma hiyo sanjari na elimu ya afya itakayowasaidia kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.

 Katika kuadhimisha siku ya moyo dunia ambayo kauli mbiu yake ni “fanya  uamuzi sahihi kuhusu moyo wako” wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC wanafanya kambi maalum ya siku tano iliyoanza tarehe 26 hadi 30 mwezi huu ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani.



Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa