Watoto 77 wafanyiwa upasuaji wa moyo ndani ya wiki moja
Naibu Balozi wa Saud Arabia Nchini Tanzania Mhe.
Abdallah Al - Harbi akiwapongeza madaktari kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha
Misaada ya kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia kwa ushirikiano wanaoufanya
katika kutoa huduma za matibabu ya moyo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyomalizika leo katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa wagonjwa waliolazwa katika chumba
cha uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Saudi Arabia Loay Abdulsamad akieezea
matibabu waliyoyatoa kwa watoto wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu
kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa
kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu
kilichopo nchini Saudi Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Mashiriki ya Kati kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Hemedi Mgaza akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya
moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao
kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo nchini Saudi
Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo Jijini
Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo kwa watoto
kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiwashukuru
madaktari kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo
nchini Saudi Arabia kwa kuendelea kushirikiana na madaktari wa JKCI wakati wa
mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto
iliyofanywa na madakari hao na kumalizika leo katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam wa afya wakifuatili yaliyokuwa
yakiendelea wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya
matibabu ya moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo
nchini Saudi Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam wa afya wakifuatili yaliyokuwa
yakiendelea wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya
matibabu ya moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa kushirikiana na
wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo
nchini Saudi Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mama wa Mtoto aliyefanyiwa Upasuaji mkubwa wa moyo kutoka
Mkoani Kigoma Hadija Yusufu akitoa neno la shukrani kwa madaktari waliomfanyia
upasuaji mtoto wake wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi
maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa
kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu
kilichopo nchini Saudi Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Balozi wa Saud Arabia Nchini Tanzania Mhe. Abdallah Al – Harbi katika picha ya pamoja na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia baada ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Khamis Mussa
**************************************************************************************************
Watoto 77 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya
matibabu ya moyo iliyofanywa na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya
Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia
Katika kambi hiyo watoto 47 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa
moyo kupitia tundu dogo kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab na watoto
wengine 30 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji katika
kambi hiyo waliokuwa na matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na
mishipa ya damu ya moyo kutokuwa katika mpangilio maalum.
“Wagonjwa 77 kwa muda wa wiki moja kufanyiwa upasuaji sio
kitu kidogo, Taasisi nyingi zinazofanya upasuaji wa moyo inaweza kuwachukua
mwaka mmoja kumaliza watoto 77, nawapongeza wataalam hawa kwa kazi kubwa na
nzuri waliyoifanya kwa wiki moja”,
“Wataalam kutoka nchini Saudi Arabia wamekuja na vifaa vya
kisasa ambavyo huwa tunavitumia na gharama zake huwa ni kubwa lakini kupitia
kambi hii tumeweza kuwafanyia upasuaji watoto ambao wanatoka kwenye familia zisizokuwa
na uwezo hivyo kuwafanyia upasuaji wa moyo bila gharama”, alisema Prof. Janabi
Prof. Janabi alisema kuwa upasuji uliofanyika ulikua wa
mafanikio na wa hali ya juu kwani baadhi ya watoto walikua na uzito mdogo kama
kilo nne hivyo kufanya matibabu hayo kutokuwa rahisi lakini kupita wataalam hao
watoto wote 77 wamefanyiwa upasuaji bila kupoteza mtoto hata mmoja.
“kipitia kambi hii maalum ya matibabu ya moyo watoto wamepata
nafasi ya kuendelea kuishi maisha ambayo hayatakuwa na changamoto za magonjwa
ya moyo kwani upasuaji waliofanyiwa unafanyika mara moja na mtoto anapona
kabisa”,
“Kwa niaba ya wataalam wenzangu nawashukuru sana Wizara ya
Afya, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha wataalam hawa kuendelea kuja na
kutoa huduma ya matibabu kwa watoto wenye magonjwa ya moyo wanaohitaji
upasuji”, alisema Prof Janabi
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha
Mahita amewapongeza madaktari kutoka nchini Saudi Arabia kwa kuendelea kutoa
msaada wa matibabu kwa watoto wenye uhitaji wa matibabu ya moyo na ujuzi
wanaoutoa kwa wataalam wa afya hapa nchini hivyo kuboresha huduma za afya hasa
huduma ya upasuaji wa moyo kwa watoto.
“Kwetu sisi Wizara haya ni mafanikio makubwa sana yamefanyika
kwa kipindi kifupi kuokoa maisha ya watoto wetu, Kambi maalum za matibabu zina
manufaa sana kwani hutusaidia kupata ujuzi zaidi na kujenga mahusiano baina ya
nchi yetu na nchi ambazo wamekua nasi katika kubadilishana ujuzi wa kitabibu”,
alisema Dkt. Asha
Akizungumza wakati wa mkutano huo Daktari wa wagonjwa
waliolazwa katika Chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) Loay
Abdulsamad alisema kuwa wataalam kutoka Saudi Arabia wamekua na uhusiano na
JKCI kwa kipindi cha miaka saba uhusiano ambao umeleta mafanikio makubwa na
kuongeza ujuzi kwa wataalam hao.
“Tunafanya kambi za matibabu ya moyo katika nchi mbalimbali
lakini tunajisikia furaha kufanya kambi hizi hapa Tanzania kutokana na ukarimu
wa watu wake lakini pia wataalam wa hapa ujuzi wao umekua ukiongezeka kwa kasi
tofauti na tulivyoanza uhusiano huu wa kubadilishana ujuzi katika kutoa tiba
mwaka 2015”,
“Tutaendelea na kambi za matibabu ya moyo kwa watoto hapa
JKCI tukiwa na lengo la kuwasaidia watoto ambao wanatoka katika familia
zisizokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ili watoto hao nao waweze
kupata nafasi nyingine ya kuishi bila ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo”, alisema
Dkt. Abdulsamad
Akitoa neno la Shukrani Mzazi ambaye mtoto wake amefanyiwa
upasuaji mkubwa wa moyo katika kambi hiyo Hadija Yusuph mkazi wa Kigoma
amewashukuru wataalam hao kwa kuokoa maisha ya mtoto wake baada ya kuhangaika
kwa muda mrefu bila ya kujua tatizo alilonalo mwanaye hadi alipofika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete kwa ajili ya matibabu.
“Nawashukuru sana madaktari ambao wamepambania maisha ya
mtoto wangu ambaye hapo awali hatukujua anasumbuliwa na nini hadi tulipofika
JKCI, sasa naona mabadiliko baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo nawashukuru
sana”, alisema Hadija
Comments
Post a Comment