Mamia wajitokeza JKCI kufanyiwa upimaji wa magonjwa ya moyo


Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam akisoma jarida la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari bila malipo katika kuadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam

Mtafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Neema Kailembo akimfanyia usajiri mwananchi aliyefika kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete leo Jijini Dar es Salaam 

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happy Mulagwa akimpima wingi wa sukari mwilini mwananchi aliyefika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo Jijini Dar es Salaam.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mali Sabuni akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo Jijini Dar es Salaam


Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Felister Mgare akimsikiliza mwananchi aliyefika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo Jijini Dar es Salaam

Mfamasia kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Zydus Salome Vitali akimwelezea namna ya kutumia dawa mwananchi aliyefika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa kuadhimisha siku ya moyo duniani leo Jijini Dar es Salaam

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akizungumza na baadhi ya wagonjwa waliowahi kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari bila malipo katika kuadhimisha siku ya moyo duniani iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam


 Mjumbe kutoka chama Moyo ni Uhai (MOU) kinachowaunganisha wagonjwa waliowahi kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Kabila Mbwama akiwaonesha wagonjwa wa moyo waliolazwa katika Taasisi hiyo sehemu aliyofanyiwa upasuaji wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo na kisukari katika kuadhimisha siku ya moyo duniani leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam

Picha na Khamis Mussa

*****************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa