Bodi ya Wadhamini ya JKCI yasomewa makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24
Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi Bugando (CUHAS) Prof. William Mahalu akiongoza kikao cha pili cha Bodi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge akitoa taarifa ya utendaji wa kazi zilizofanywa na taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Oktoba hadi Desemba 2022 katika mwaka wa fedha wa 2022/23 katika kikao cha pili cha Bodi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA.Godfrey Kilenga ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ,TAB Consult akichangia mada wakati wa kikao cha pili cha Bodi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Afya ya
Uzazi na Mtoto Mkoa wa Rukwa akipitia
kitabu cha taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi
mitatu ya Oktoba hadi Desemba 2022 wakati wa kikao cha pili cha Bodi hiyo kilichofanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Taasisi hiyo Prof. Wiliam Mahalu wakati wa kikao cha pili cha bodi hiyo
kilichofanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Comments
Post a Comment