Wakazi wa Dodoma washukuru huduma ya upimaji magonjwa ya moyo
Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakiwapima wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo shinikizo la damu na kiwango cha sukari mwilini wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya siku tatu ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adam Ndamayape akitoa elimu ya jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayoenda sambamba na maonesho ya siku tatu ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Wakazi wa mkoa wa Dodoma wameishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa
kutoa huduma za upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo pamoja na ushauri wa
jinsi ya kuyaepuka magonjwa hayo bila malipo yoyote yale.
Huduma
hiyo inatolewa katika maadhimisho ya miaka 70 ya baraza la uuguzi na ukunga
yanayoenda sambamba na maonesho ya huduma zinazotolewa na wauguzi yanayofanyika
katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi waliofika katika banda la JKCI kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo na kupata ushauri walisema elimu waliyoipata ni nzuri na
imewasaidia kuwapa uelewa wa kutosha kuhusu magonjwa ya moyo na jinsi ya
kuepukana nayo.
Mama
Amina Ismail mkazi wa Makole alisema huduma aliyoipata kutoka kwa wauguzi ni
nzuri na imemsaidia kufahamu shinikizo lake la juu na la chini la damu likoje
kwani hii ni mara ya kwanza kupima kwa hiari kiwango cha sukari mwilini na
shinikizo la juu la damu.
“Licha
ya kufanya vipimo, nimepata elimu ya lishe bora ambayo imenifungua akili na kufahamu
aina gani ya vyakula natakiwa kuvila ili vinisaidie kujenga mwili pamoja na
kulinda moyo wangu ili uwe salama”,.
“Elimu
ya lishe ni nzuri ninatoa ushauri kuwe na vipindi kama hivi redioni ili watu
wengi zaidi waweze kupata ujumbe huu kwani wengi wetu wakiwemo watoto
tunakunywa vinywaji vya kusindika zikiwemo soda na juisi bila kujua kuwa
vinamadhara mwilini”, alisema Mama Amina.
Naye
Emmanuel Jembe mkazi wa Chamwino alisema baada ya kutembelea katika banda hilo
ameweza kupata elimu ya jinsi ya kutambua dalili za shambulio la moyo na
madhara yake kwani hapo awali hakuwa anajua chochote kuhusu dalili za ugonjwa
huo na kusema kuwa hivi sasa ameweza
kufahamu vizuri.
“Nimefahamu
kuwa ugonjwa wa shambulio la moyo ni hatari kwani unaua na dalili za ugonjwa
huu ni maumivu ya kifua upande
wa kushoto, kifua kubana kushindwa kupumua na wakati mwingine maumivu ya tumbo.
Nitaenda kutoa elimu hii kwa wenzangu ili waonapo dalili hizi wawahi hospitali
mapema” , alisema.
Akitoa elimu ya jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo Afisa Uuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adam Ndamayape alisema magonjwa ya moyo ni moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi, kutotumia bidhaa za tumbaku, kutokunywa pombe kupitiliza, kula vyakula bora na kufanya mazoezi.
Comments
Post a Comment