Posts

Showing posts from August, 2023

JKCI Dar Group yaboresha huduma ya dharura

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiangalia namna ambavyo wataalamu wa afya wa JKCI Dar Group wakifanya mazoezi kwa vitendo ya namna ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha wagonjwa wa dharura katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam Daktari wa usingizi na mkuu wa timu ya kuratibu jinsi ya kuokoa wagonjwa wa dharura wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge akimuonyesha mtaalamu wa afya wa Hospitali ya JKCI Dar Group namna ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura wakati wa uzinduzi wa kitengo cha wagonjwa wa dharura katika Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitengo cha wagonjwa wa dharura kilichopo Hospitali ya JKCI Dar Group leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akielezea huduma zinazotole

Upimaji magonjwa ya moyo JKCI Dar Group

Image

Watu 700 wapimwa moyo Kilimanjaro

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kawajika Mwinyipembe akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Arusha aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa afya JKCI na wenzao wa MRRH na kumalizika jana Mkoani Kilimanjaro. Jumla ya watu 700 wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimpa maelekezo ya namna ya kutumia dawa mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi  maalum ya upimaji na matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa afya JKCI na wenzao wa MRRH na kumalizika jana Mkoani Kilimanjaro. Jumla ya watu 700 wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo. Afisa Uuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Zaituni Mbowe akimpima urefu na uzito mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mko

JKCI wamuaga Prof. Mahalu

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisukuma toroli lililobeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Marehemu Prof. William Mahalu ambaye pia alikuwa daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wakielekea kwenye ibada ya kumuaga iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Muhimbili. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wanataaluma ya afya wakiwa katika ibada ya kumuaga  aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Marehemu Prof. William Mahalu iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Muhimbili. Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimfariji mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Marehemu Prof. William Mahalu wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili l

Waishukuru JKCI kwa kuwasogezea huduma za matibabu ya moyo

Image
Daktari bingwa wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanyakazi (Echocardiograph – ECHO) mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akizungumza na mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI na wenzao wa MRRH Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akimsikiliza mwananchi wa mkoa wa Kilimanjaro akijibu maswali ya ufahamu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRR

7000 wafikiwa na huduma ya tiba mkoba

Image

Zaidi ya wananchi 7000 wafikiwa na huduma ya tiba mkoba

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH. Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Anandumi Mmari akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kilalo Barati akimpima shinikizo la damu mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ma

Mamia wajitokeza kupima moyo Kilimanjaro

Image
Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani wakisubiria kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magdalena Chikawe akimpima sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya na mwenzake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Benson Towo wakimsikiliza mwananchi aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maaalum ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka JKCI na wenzao wa MRRH. Afisa

JKCI wamlilia Prof. Mahalu

Image
  Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akimkabidhi begi lenye vitendea kazi aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu mara baada ya kuizindua bodi hiyo Agosti mwaka jana jijini Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya    Kikwete (JKCI) ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Prof. Wiliam Mahalu akimsikiliza Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge wakati wa  kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika mwishoni mwa mwaka jana    jijini Dar es Salaam. ********************************************************************************************************************************************* Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Prof. William Mahalu aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo na mmoja wa madaktari bingwa wa moyo wa kwanza h

JKCI kushiriki Kongamano la nane la dunia la wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto nchini Marekani

Image
 ************************************************************************************************************************ Na: Stella Gama – Dar es Salaam Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto watano kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kushiriki Kongamano la nane la dunia la watoa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto linalofanyika nchini Marekani. Kongamano hilo linatarajiwa kuanza tarehe 28 agosti hadi 3 septemba 2023 ambapo jumla ya washiriki zaidi ya 4500 kutoka nchi mbalimbali duniani kushiriki. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Daktari bingwa wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naizhijwa Majani alisema kongamano hilo hufanyika kila baada ya miaka minne ambapo mara ya mwisho lilifanyika mwaka 2017 Barcelona nchini Spain. “JKCI iliweza kushiriki katika kongamano la saba lililofanyika nchini Spain na kujifunza kuhusu msingi wa data shirikishi wa uboreshaji wa ubora wa huduma kimataifa (International Quality Improveme

Waishukuru JKCI Dar Group kwa huduma bora waliyoitoa kwa mzazi wao

Image
Rose Mtono anayeishi nchini Ujerumani akiwa katika picha ya pamoja na wadogo zake na wafanyakazi wa JKCI Dar Group walipofika katika Hospitali hiyo iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwashukuru wafanyakazi hao kwa huduma bora waliyoitoa kwa baba yao wakati wanamtibu

Toeni huduma bora kwa wagonjwa

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kupitia utekelezaji wa kazi zilizofanyika kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Daktari wa usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge akielezea namna kitengo cha usingizi kinavyofanya kazi wakati wa kikao cha kupitia utekelezaji wa kazi zilizofanyika kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau akielezea namna kitengo cha Ubora wa Huduma kinavyosimamia utekelezaji wa majukumu kwa idara na vitengo wakati wa kikao cha kupitia utekelezaji wa kazi zilizofanyika kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adam Sembe akich

Milioni 100 zatolewa matibabu ya moyo kwa watoto

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge hundi ya shilingi milioni 100 iliyotolewa leo katika Viwanja vya Farasi Oyster bay jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB fedha zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwaongoza viongozi wengine katika matembezi ya kilometa 5 wakati wa mbio za CRDB Marathon kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI na wanawake wenye ujauzito hatarishi wanaotibiwa CCBRT leo jijini Dar es Salaam.  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya na Afisa Uuguzi wa Taasisi hiyo Benson Bisare wakimsikiliza mwananchi aliyeshiriki mbio za CRDB Marathon kabla ya kumpatia huduma wakati wa mbio hizo zilizofanyik

Wafanyakazi bora watunukiwa

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo Afisa Muuguzi mstaafu wa Taasisi hiyo Mary Haule wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mfanyakazi bora wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 aliyeshika nafasi ya kwanza afisa Uuguzi Samweli mpiga akipokea ngao ya mfanyakazi bora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi hao iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mfanyakazi bora wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023 aliyeshika nafasi ya pili Fundi Sanifu wa Moyo Jasmine Keria akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi hao iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Da

Wagonjwa 10 wazibuliwa mishipa ya damu iliyoziba na kuusababishia moyo kushindwa kufanya kazi vizuri

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na mwenzao kutoka Hospitali ya Max iliyopo nchini India Dkt. Subhash Sinha kupandikiza mshipa wa damu katika moyo wakati wa kambi maalum ya siku saba ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa ambao mishipa yao ya damu imeziba na kiwango cha ufanyaji kazi wa moyo kipo chini ya asilimia 30. Jumla ya wagonjwa 10 wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo iliyoanza jumatatu na kumalizika leo jijini Dar es Salaam. Na: JKCI ********************************************************************************************************** Wagonjwa 10 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kuzibua mishipa ya damu iliyoziba katika kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku saba.   Kambi hiyo iliyomalizika leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam imefanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa JKCI kwa kushirikiana na mwenzao kutoka Hospitali y