Mamia wajitokeza kupima moyo Kilimanjaro


Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani wakisubiria kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magdalena Chikawe akimpima sukari kwenye damu mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH. 


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya na mwenzake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Benson Towo wakimsikiliza mwananchi aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maaalum ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa afya kutoka JKCI na wenzao wa MRRH.


Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji na mwenzake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi Ester Wazoel wakimpatia ushauri wa lishe mkazi wa Kilimanjaro aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa MRRH.

****************************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari