Posts

Showing posts from October, 2023

Wapigwa msasa wa kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo sugu ya hitilafu ka...

Image

Wapigwa msasa wa kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo sugu ya hitilafu katika msukumo wa damu na utengenezaji wa mapigo ya moyo

Image
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Chuo Kikuu cha Brescia kilichopo nchini Italia kumfanyia upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab mgonjwa ambaye ana matatizo ya hitilafu katika msukumo wa damu wakati wa kambi maalumu ya siku tatu iliyoanza leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Na: JKCI ********************************************************************************************************* Wataalamu wa magonjwa ya moyo na  mfumo wa umeme wa moyo  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanapewa mafunzo kwa vitendo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo sugu ya hitilafu katika msukumo wa damu na utengenezaji wa mapigo ya moyo. Mafunzo hayo ya siku tatu yanatolewa na Prof. Antonio Curnis ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mfumo wa umeme wa moyo kutoka chuo kikuu cha Brescia kilichopo nchni Italia. Prof. Curnis alisema lengo la mafunzo ha

Jengo jipya la JKCI kujengwa Mloganzila

Image
Wajumbe kutoka Serikali ya Watu wa China wakiangalia jiwe la msingi lililowekwa katika jengo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kukutana na uongozi wa JKCI kujadiliana kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo jipya la JKCI mwishoni mwa mwaka huu litakalojengwa eneo la mloganzila. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Tatizo Waane akizungumza wakati wa kikao na wajumbe kutoka Serikali ya Watu wa China walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kujadiliana kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo jipya la JKCI mwishoni mwa mwaka huu litakalojengwa eneo la mloganzila. Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Liggyle Vumilia akizungumza wakati wa kikao na wajumbe kutoka Serikali ya Watu wa China walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kujadiliana kabla ya kuanza kwa ujenzi wa jengo jipya la JKCI mwishoni mwa mwaka huu litakalojengwa eneo la mloganzila. Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi

JKCI wapatiwa msaada wa viti mwendo 10 vya wagonjwa

Image
Daktari kutoka kampuni inayojishughulisha na masuala ya afya Stufit Africa PVT Ltd Shujat Haider akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo viti mwendo 10 vilivyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya kuhudumia wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akipokea hati ya umiliki wa viti mwendo 10 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa kampuni inayojishughulisha na masuala ya afya Stufit Africa PVT Ltd Mehdi Surani baada ya kukabidhi viti hivyo. Picha na: JKCI ******************************************************************************************************************

JKCI kushirikiana na chuo kikuu cha New York cha nchini Marekani katika matibabu ya moyo na utafiti wa magonjwa ya moyo

Image
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Kituo cha Utafiti Ifakara na wenzao wa Chuo Kikuu cha New York kilichopo nchini Marekani wakiwa katika kikao cha kujadili vipaumbele vya mahusiano kati ya JKCI na Chuo hicho kuhusiana na masuala ya utafiti, elimu na utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, viongozi wengine wa JKCI na viongozi wa Kituo cha Utafiti Ifakara wakimsikiliza mtaalam wa afya kutoka Chuo Kikuu cha New York kilichopo nchini Marekani akiwaonesha namna ambavyo wanatoa mafunzo kwa wanafunzi wa Udaktari walipotembelea chuo hicho kwaajili ya kujadili maeneo ya kushirikiana katika masuala ya utafiti, elimu na utuoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo. Mtaalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha New York kilichopo nchini Marekani akiwaelezea viongozi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Kituo cha Utafiti Ifaraka namna ambavyo chuo hicho kinafanya kazi wakati viongozi hao wa

Wapewa mafunzo ya kutambua viashiria vya hatari katika utendaji kazi

Image
Mkufunzi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Indiael Kaaya akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) namna ya kutambua viashiria mbalimbali vinavyoweza kusababisha hatari katika utendaji wa kazi vinavyoweza kujitokeza katika mazingira na sura mbalimbali wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika hivi karibuni. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Martin Rubamba akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kutambua viashiria mbalimbali vinavyoweza kusababisha hatari katika utendaji wa kazi vinavyoweza kujitokeza katika mazingira na sura mbalimbali kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa JKCI hivi karibuni. Mteknolojia wa Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mariam Steven akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kutambua viashiria mbalimbali vinavyoweza kusababisha hatari katika utendaji wa kazi vinavyoweza kujitokeza katika mazingira na sura mbalimbali kwa wafanyakazi wa Taasisi hiy

Wataalamu wa JKCI wajifunza upasuaji wa kubadilisha Valvu bila kufungua kifua

Image
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa nchini India wakifanya upasuaji mdogo wa moyo kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic  Valve Implantation procedure – TAVI) wakati wa mafunzo ya siku tano kwa wataalamu hao yanayoendelea nchini India.                                                                                                                               Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa nchini India wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya upasuaji mdogo wa moyo kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) bila kufungua kifua (Transcatheter Aortic  Valve Implantation procedure – TAVI) wakati wa mafunzo ya siku tano kwa wataalamu hao yanayoendelea nchini India. Picha na: JKCI **********************************************************************************************

JKCI yawapeleka wataalamu wake nchini India kujifunza upasuaji wa kubadilisha Valvu bila kufungua kifua

Image
Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa  nchini India kwaajili ya kujifunza upasuaji wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) pasipo kufanya upasuaji wa kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI). Upasuaji huo unafanyika kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab ambao ni maabara inayotumia mionzi maalumu kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo. ************************************************************************************************************************************************************************************************************** Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wako nchini India kwaajili ya kujifunza upasuaji wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu (Aortic Valve) pasipo kufanya upasuaji wa kufungua kifua (Transcatheter Aortic Valve Implantation procedure – TAVI).

Kwa mara ya kwanza JKCI Dar Group wafanya upasuaji mdogo wa moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Samweli Rweyemamu akimfanyia upasuaji mdogo wa moyo kuondoa maji yaliyopo katika mfuko wa kutunza moyo mgonjwa ambaye moyo wake umejaa maji hivi karibuni katika Hospitali hiyo. **************************************************************************************************** Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group imefanya upasuaji mdogo wa moyo kuondoa maji yaliyokuwa yameuzunguka moyo kwa wagonjwa ambao walikuwa na tatizo la maji kujaa kwenye mfuko unaotunza moyo (pericardia effusion). Upasuaji huo umefanyika kwa wagonjwa wawili ambao wameonekana kuwa na dalili za magonjwa mengine yaliyopelekea mfuko unaotunza moyo kujaa maji kwa kiwango kikubwa. Akizungumza kuhusu matibabu hayo Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete tawi la JKCI Hospitali ya Dar Group Samweli Rweyemamu alisema wagonjwa hao maji yamekuwa yakijaa

Milioni 950 zaokolewa kwa watoto 37 kufanyiwa upasuaji nchini

Image
Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mtoto mpasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab kufungua mshipa wa damu uliobana wakati wa kambi maalum ya siku tano iliyomalizika jana jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 37 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo. Na: JKCI ************************************************************************************************************ Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa kiasi cha shilingi milioni 950 ambazo Serikali ingetumia kama watoto 37 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wangepelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo. Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirikal la Mending Kids lililopo nchini Marekani Daktari bingwa wa upasujai wa moyo kwa watoto wa JKCI Godwin Sh

Wafanyakazi JKCI wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia utaalamu walionao kuwahudumia wagonjwa

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akikata keki ya kuadhimisha miaka nane tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo wakati wa mafunzo ya jinsi ya kufanya kazi kimkakati na kufikia malengo waliyojiwekea kwa wafanyakazi wa JKCI yaliyofanyika hivi karibuni katika msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Kisarawe mkoani. Mkufunzi kutoka Taasisi ya Uongozi Institute Dunstan Mulaku akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi ya kufanya kazi kimkakati na kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika hivi karibuni   katika msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo Kisarawe mkoani Pwani. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi zawadi ya mfano wa hundi ya shilingi milioni 11.1 Afisa Uuguzi  Mstaafu Fatihiya Mustafa wakati wa mafunzo kwa wafanyakazi ya jinsi ya kufanya kazi kimkakati na kufikia malengo waliyojiwekea yaliyokwenda sambamba na ha

Watoto 45 kufanyiwa upasuaji wa moyo

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano iliyoanza jana. Jumla ya watoto 45 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo  Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Mendingi Kids la nchini Marekani wakimfanyia mtoto upasuaji wa tundu dogo kuziba tundu lililopo kwenye moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano iliyoanza jana. Jumla ya watoto 45 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Mendingi Kids la nchini Marekani wakiandaa vifaa vitakavyotumika kwenye upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa cathlab kwa mtoto ambaye mishipa yake ya damu imebana wakati wa kambi   maalumu ya siku tan

Wafanyakazi JKCI wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia utaalamu walionao kuwahudumia wagonjwa

Image

JKCI wafanya utalii wa ndani msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi

Image
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika lango la kuingia kwenye msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo  Kisarawe mkoani Pwani walipotembelea msitu huo hivi karibuni kwaajili ya  kufanya utalii wa ndani na kujionea vivutio vilivyopo katika msitu huo. Muongoza Watalii kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Peter Masome akiwaeleza Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya miti ya asili iliyopo ndani ya  msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo  Kisarawe mkoani Pwani wakati wafanyakazi hao walipofanya utalii wa ndani hivi karibuni katika msitu huo. Muongoza Watalii kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Omary Sharif    akiwaeleza Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya vivutio vilivyopo ndani ya    msitu wa mazingira asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo    Kisarawe mkoani Pwani wakati wafanyakazi hao walipofanya utalii wa ndani mwishoni mwa wiki iliyopita. ******************************************************