Watu 604 wapimwa moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Mobhare Matinyi akiongoza matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.
Kikundi cha Wasafi Jogging wakiwa katika matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuanzia uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa katika matembezi ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo. Matembezi hayo ya umbali wa kilometa nne yalifanyika hivi karibuni kuanzia uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group.
Baadhi ya wananchi waliopata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) hospitali ya Dar Group wakipewa dawa za kutibu maradhi mbalimbali waliyokutwa nayo. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akitoa ushauri wa jinsi ya kutumia dawa za moyo kwa mwananchi aliyefika JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa.
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maclina Komba akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akichukuwa taarifa za mwananchi aliyefika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Moyo Tanzania (TCS) Robert Mvungi akisikiliza mwananchi aliyefika JKCI Hospitali ya Dar Group kwaajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani. Watu 604 walipata huduma za matibabu kati yao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na mfumo wa umeme wa moyo na 58 wanahitaji kupata matibabu ya kibingwa.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe bora kwa wananchi waliofika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Watu 604 Wamepata huduma za upimaji na matibabu ya
moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo duniani yaliyofanyika katika
Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group
iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar
es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu
alisema upimaji huo ulifanyika kwa muda wa siku mbili ambapo wananchi walipata
huduma za upimaji, ushauri pamoja na kupewa dawa kwa wale waliokutwa na
matatizo.
Dkt. Shemu alisema mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa na
kuwaomba wananchi wakati mwingine watakaposikia kuna upimaji wa magonjwa
mbalimbali unafanyika mahali wasiache kwenda kupima afya zao.
”Watu 604 walifanyiwa vipimo vya awali vya magonjwa ya moyo kati
ya hao 99 walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi pamoja
na mfumo wa umeme wa moyo na 58 tumewakuta na matatizo ya moyo yanayohitaji
matibabu ya kibingwa tumewapa rufaa ya kuja kutibiwa JKCI”,.
“Wagonjwa wengi
tumewakuta na tatizo la shinikizo la juu la damu na wengine wameshapata madhara
ya shinikizo la damu hii ikiwa ni pamoja na kutanuka kwa misuli ya moyo,
wengine mishipa yao ya damu ya moyo imeziba, kuna ambao tumewakuta na kiwango kikubwa cha
mafuta kwenye damu pamoja na matatizo mengine ya moyo”, alisema Dkt. Shemu.
Dkt. Shemu alisema gharama za matibabu ya moyo ni kubwa na
kwa asilimia 80 magonjwa hayo yanaweza kuepukika njia moja wapo ya kuyaepuka ni
kufanya mazoezi na kupima afya mara kwa mara ili kujua kama unamatatizo ya moyo
na kuanza matibabu mapema kuliko kusubiri wakati ambao moyo umepata shida na
kuanza matibabu.
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na
Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Mobhare Matinyi aliyeongoza matembezi ya
kupambana na magonjwa yasiyoambukiza alisema wilaya hiyo imejipanga kuhamasisha
jamii kufanya mazoezi na kupima afya ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na
magonjwa hayo yakiwemo ya moyo.
“Leo hii vikundi mbalimbali vya mazoezi vimetembea umbali wa
kilomita nne kutoka uwanja wa Uhuru hadi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
hospitali ya Dar Group kwa ajili ya kufanya mazoezi. Ninaipongeza JKCI kwa
kusherehekea siku ya moyo duniani kwa kufanya upimaji wa afya na kuandaa
matembezi haya”,.
“Licha ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi Wilaya ya Temeke
pia inahamasisha wananchi kufanya usafi katika mazingira yao, kupima afya na katika
matukio makubwa yanayofanyika tunawahamasisha wananchi kuchangia damu na
mwitikio huwa ni mkubwa”, alisema Mhe. Matinyi.
Mhe. Matinyi alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa kutoa fedha katika sekta ya afya ambapo sasa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) inauwezo wa kuwahudumia watanzania na wagonjwa kutoka nje ya nchi na
kuwaomba wananchi waitumie hospitali hiyo katika matibabu.
Nao wananchi
walioshiriki zoezi la upimaji na matibabu hayo ambayo yalienda sambamba na
matembezi ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza waliishukuru Serikali kwa huduma waliyoipata
na kusema imewasaidia kupata elimu na matibabu ya magonjwa ya moyo.
“Mimi ninashida ya presha nilisikia katika taarifa ya habari
kutakuwa na huduma ya upimaji nami nikaamua kuja kupima ili nione maendeleo ya
afya yangu, nashukuru sana nimepima na nimepewa dawa za kutumia huduma hii
nimeipata bila malipo yoyote yale”,.
“Huduma niliyoipata ni nzuri, ninaomba huduma hii iweze
kwenda hadi vijijini ili wananchi wengi wanaoteseka
na magonjwa ya shinikizo la damu na moyo ambao
uwezo wao kifedha ni mdogo waweze kufaidika nayo”, alishukuru Christina
Mohamed mkazi wa Gongo la Mboto.
“Mimi sina bima ya afya nilikuja na mama yangu kupima afya
namshukuru Mungu sina tatizo lolote lile la moyo ila nimekutwa na matatizo
mengine nimepewa dawa za kikohozi na mafua , ninawashauri wananchi wenzangu nao
waje kupima afya zao kwani huduma inatolewa bila malipo yoyote yale”, alisema
Emmanuel Babu mkazi wa Tabata.
Comments
Post a Comment