JKCI kushirikiana na chuo kikuu cha New York cha nchini Marekani katika matibabu ya moyo na utafiti wa magonjwa ya moyo
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Kituo cha
Utafiti Ifakara na wenzao wa Chuo Kikuu cha New York kilichopo nchini Marekani
wakiwa katika kikao cha kujadili vipaumbele vya mahusiano kati ya JKCI na Chuo hicho
kuhusiana na masuala ya utafiti, elimu na utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa
moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge, viongozi wengine wa JKCI na viongozi wa Kituo cha Utafiti
Ifakara wakimsikiliza mtaalam wa afya kutoka Chuo Kikuu cha New York kilichopo
nchini Marekani akiwaonesha namna ambavyo wanatoa mafunzo kwa wanafunzi wa Udaktari walipotembelea chuo hicho kwaajili ya kujadili maeneo ya
kushirikiana katika masuala ya utafiti, elimu na utuoaji wa huduma kwa wagonjwa
wa moyo.
Mtaalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha New York kilichopo
nchini Marekani akiwaelezea viongozi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) na wenzao kutoka Kituo cha Utafiti Ifaraka namna ambavyo chuo hicho
kinafanya kazi wakati viongozi hao walipotembela katika chuo hicho kujadili maeneo
ya kushirikiana katika masuala ya utafiti, elimu na utoaji wa huduma kwa
wagonjwa wa moyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge, viongozi wengine wa JKCI na wenzao kutoka Kituo cha Utafiti
Ifakara wakitembelea maeneo ya Chuo Kikuu cha New York kilichopo nchini
Marekani mara baada ya kikao cha kujadili maeneo ya kushirikiana katika masuala
ya utafiti, elimu na utuoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo.
Picha na: JKCI
*******************************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment