Posts

Showing posts from February, 2024

Mafunzo ya Uadilifu kutolewa kwa wafanyakazi wa JKCI

Image
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa taasisi hiyo leo wakati wa kikao cha nane cha Baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akiwasilisha makisio ya bajeti ya taasisi hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya Afya Taifa (TUGHE) Dkt. Jane Madete akichangia mada wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi wa...

Watu 587 wapimwa moyo Arusha

Image
Watu 587 wamepimwa moyo wakati wa kambi maalumu ya siku sita iliyofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mkoani Arusha. Kambi hiyo maalumu iliyomalizika hivi karibuni imefanyika katika viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) kuanzia tarehe 19 Februari ambapo wananchi wa Arusha na mikoa ya jirani walipata fursa ya kupima magonjwa ya moyo. Akizungumzia kambi hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Rweyemamu alisema jumla ya wanawake 364 sawa na asilimia 60 na wanaume 223 sawa na asilimia 40 walipatiwa huduma za vipimo na matibabu ya magonjwa ya moyo. Dkt. Rweyemamu alisema baada ya watu hao kufanyiwa vipimo na matibabu, watu 58 sawa na asilimia 10 walipewa rufaa kufika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu zaidi na wengine kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. “Asilimia 90 ya watu wote waliopatiwa matibabu katika kambi hii tumewakuta na matatizo ya shinikizo la juu...

JKCI yafanya kliniki ya matibabu ya moyo mkoani Geita

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Marsia Tillya   akiandika taarifa mara baada ya kusoma majibu ya mgonjwa aliyefika katika kliniki maalumu ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanyika   katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) iliyopo mkoani Geita. Jumla ya wagonjwa 312 wamepata huduma ya uchunguzi na matibabu katika kliniki hiyo iliyomalizika leo. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jasmine Keria akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mkazi wa Geita aliyefika katika kliniki maalumu ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanywa  na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) iliyopo mkoani Geita. Baadhi ya wakazi wa Geita wakiwa katika foleni ya kusubiri kupata huduma katika kliniki maalumu ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) iliyopo mkoani...

Kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi yatembelea JKCI

Image
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Deogratis Nkya akiwaonesha wajumbe wa kamati ya kudumu ya   bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi   jinsi wanavyofanya upasuaji wa kuzibua tundu la moyo wa mtoto bila ya kufungua kifua wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI  kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Dkt. Nkya   ni makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya   bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi aina za upasuaji wa moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo wakati kamati hiyo ilipotembelea JKCI  kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni misimamizi wa wodi ya watoto Theresia Marimo akiwaeleza wajumbe...

NHC yatakiwa kukamilisha ujenzi wa jengo la JKCI

Image
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya  bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni  akuzungumza na vyombo vya habari wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. ********************************************************************************************************************************************************************************************************************* Kamati ya kudumu ya   bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi imelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha haraka mradi wa ujenzi wa jengo la utawala na vipimo la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Makamu   Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni   wakati wa ziara ya kamati hiyo waliyoifanya JKCI kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matiba...

Wagonjwa 10 wafanyiwa upasuaji wa moyo

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu mgonjwa ambaye mshipa wake ulikuwa umeziba ((Coronary Artery Bypass Graft Surgery – CABG) wakati wa kambi maalumu ya siku nne iliyomalizika hivi karibuni katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 10 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ************************************************************************************************************ Wagonjwa 10 wenye matatizo ya mishipa ya damu kuziba, valvu za moyo kuziba pamoja na mshipa mkubwa wa moyo kutanuka (Coronary Artery Bypass Graft Surgery – CABG) wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu ya moyo.  Kambi hiyo maalumu ya siku nne iliyomalizika hivi karibuni imefanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi wa Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrik...

Kliniki maalumu za matibabu ya moyo na mishipa ya damu mkoani Geita

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayetoa huduma katika kliniki maalumu ya VIP Grace Mbanga akimpima sukari kwenye damu mkazi wa Geita wakati wa maonesho ya sita ya kitaifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita *********************************************************************************************************  

Kambi maalumu ya upasuaji kupitia tundu dogo kwa magonjwa ya mishipa ya damu (Aortic Diseases)

Image
Wataalamu wa upasuaji wa moyo ana mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha Valvu iliyokuwa haipitishi damu vizuri **********************************************************************************************************************  

Short Course: Competence based critical care, emergency nursing and competent based dialysis nursing

Image
 

Wagonjwa 25 kufanyiwa upasuaji wa moyo

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mshipa wa damu mgonjwa ambaye mshipa wake ulikuwa umeziba ((Coronary Artery Bypass Graft Surgery – CABG) wakati wa kambi maalumu ya siku nne iliyoanza leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 15 wanatarajia kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakivuna mshipa wa damu kwenye mguu wa mgonjwa utakaopandikizwa katika mishipa ya damu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya upasuaji mkubwa wa moyo inayofanywa na wataalamu hao kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika lililopo nchini Marekani Madaktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika lililopo nchini Marekani kumfanyia upasuaji wa tundu dogo mgonjwa ambaye mshipa wake w...

JKCI kushirikiana na Zanzibar kuanzisha kitengo cha moyo Hospitali ya Lu...

Image

JKCI kushirikiana na Zanzibar kutibu wagonjwa wa moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimwelezea huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alipotembelea banda hilo kabla ya kufunga mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo leo katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hessein Ali Mwinyi akizungumza na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo kutoka nchi 30 wakati wa kufunga mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo uliofanyika kwa siku mbili katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akimkabidhi zawadi iliyotolewa na Taasisi hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa kufunga mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo leo katika ukumbi wa Golden Tulip uliopo mjini Zanzibar Rais wa ...

Mataifa 30 wahudhuria mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika kwa siku mbili katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi tuzo ya ushirikiano mzuri na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mkurugenzi Mtendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo leo katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchini Marekani Mazen Albaghdadi akitoa mada juu ya magonjwa ya moyo wakati wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika kwa siku mbili katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo mjini Zanzibar. Madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China wanaofanya kazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia wakati wa Mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo unaofanyika kwa siku mbili katika Hotel ya Go...