Madaktari wa China wapokelewa JKCI

Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akizungumza na wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Watu wa China walivyowasili katika Taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili ya kushirikiana na wenzao wa JKCI kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wagonjwa wanaotibiwa na Taasisi hiyo. Jumla ya wataalamu wa afya watatu wanatarajia kufanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili. 
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala  na mratibu wa ushirikiano wa kimataifa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Liggyle Vumilia akiwatambulisha wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Watu wa China watakaofanya kazi JKCI walipowasili katika taasisi hiyo hivi karibuni. Jumla ya wataalamu wa afya watatu wanatarajia kufanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili.


 

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa