Kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi yatembelea JKCI
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Deogratis Nkya akiwaonesha wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi jinsi wanavyofanya upasuaji wa kuzibua tundu la moyo wa mtoto bila ya kufungua kifua wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kulia kwa Dkt. Nkya ni makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi aina za upasuaji wa moyo zinazofanyika katika Taasisi hiyo wakati kamati hiyo ilipotembelea JKCI kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni misimamizi wa wodi ya watoto Theresia Marimo akiwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi huduma za matibabu ya moyo wanazozipata watoto waliolazwa katika wodi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwaongoza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi kwenda kuona ujenzi wa jengo la utawala na vipimo unavyoendelea. Kushoto kwa Mkurugenzi ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Mbunge wa Kigamboni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea JKCI kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na Khamisi Mussa
Comments
Post a Comment