Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa taasisi hiyo leo wakati wa
kikao cha nane cha Baraza kilichofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akiwasilisha makisio ya bajeti ya taasisi hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya
Afya Taifa (TUGHE) Dkt. Jane Madete akichangia mada wakati wa kikao cha nane
cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Msaidizi wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Theresia Marombe akifafanua jambo wakati wa kikao cha nane cha baraza la
wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam.
Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Said Mselem
akitoa maoni yake wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari
wa Usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge akitoa
maoni yake wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika
leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Joachim Assenga akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja za idara hiyo wakati wa kikao
cha nane cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi
hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Naizhijwa Majani akitoa taarifa ya ukaguzi wa namna huduma
zinavyotolewa katika taasisi hiyo wakati wa kikao cha nane cha baraza la
wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia
hoja zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa kikao cha nane cha baraza la
wafanyakazi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam.
***************************************************************************************************
Wafanyakazi Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kushiriki katika mafunzo ya uadilifu ya mara kwa mara kuendelea kuifanya taasisi hiyo kuwa na ubora katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa moyo.
Mafunzo hayo ya uadilifu yanatarajiwa kutolewa kwa wafanyakazi wote kwa awamu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuongeza umahiri katika kutekeleza majukumu ya kazi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha nane cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge alisema ubora wa huduma unaotolewa na taasisi hiyo umeifanya taasisi kujulikana kimataifa hivyo hana budi kuendelea kuwapeleka watumishi wa taasisi hiyo katika mafunzo ya uadilifu mara kwa mara kuipa hadhi taasisi.
“Idara ya Utawala na Rasilimali watu hakikisheni mafunzo ya uadilifu yanatolewa kwa wafanyakazi wote kila mwaka kwani uadilifu uliopo kwa wafanyakazi ndio unaochangia kuikuza taasisi yetu”, alisema Dkt. Kisenge
Aidha Dkt. Kisenge amewataka wafanyakazi wa Taasisi hiyo kutumia uwezo walionao kutengeneza vipato vyao na kuwataka kujiunga na SACCOS ya taasisi hiyo inayoendeshwa na wafanyakazi kwani imekuwa na msaada kwa wafanyakazi wengi.
“SACCOS ya Taasisi ni moja ya sehemu sahihi ambayo mtumishi anaweza kutatua changamoto zake kwani inaendeshwa kiuadilifu tofauti na SACCOS nyingine za mitaani ambazo mtu anaweza kupoteza haki yake”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Sekta ya Afya Taifa (TUGHE) Dkt. Jane Madete aliwapongeza wajumbe wa baraza na wafanyakazi wote wa JKCI kwa kazi nzuri wanayoifanya kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji matibabu ya moyo.
“Nyinyi mlioko humu ndani mnaweza msione kile mnachokifanya lakini sisi tuliopo nje tunatambua mchango mkubwa kwa taifa mnaofanya, mmekuwa wa msaada mkubwa sana kwani wale waliokuwa wanatakiwa kwenda nje ya nchi na hawana uwezo sasa wanatibiwa JKCI”, alisema Dkt. Madete
Dkt. Madete alisema kutokana na uwepo wa uongozi mzuri katika Taasisi hiyo wajumbe wa baraza la wafanyakazi wamekuwa na hali ya kuchangia hoja zilizokuwa zikitolewa wote wakiwa na lengo la kuijenga taasisi hiyo.
“Viongozi wa Taasisi na wafanyakazi wote kwa pamoja mna maono makubwa ya kupanua taasisi hii na kuweka wigo mpana wa kutoa huduma, jinsi mnavyofanya kazi mnatembea kwenye nyayo za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetamani huduma hizi ziwafikie watanzania kwa ukaribu na kwa urahisi”, alisema Dkt. Madete
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa baraza hilo wameupongeza uongozi wa taasisi hiyo kuendesha baraza tofauti na ambavyo mabaraza mengine yamekuwa yakiendeshwa.
Afisa Uuguzi wa JKCI Flora Kasembe alisema baraza hilo limeweza kupitia hoja mbalimbali zilizotolewa na wafanyakazi ambapo baadhi ya hoja zilipatiwa ufumbuzi muda wa kikao na nyingine kuahidiwa kufanyiwa kazi kabla ya kikao kijacho.
Hamis Mndeme ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii JKCI alisema mkutano wa baraza hilo umefanyika vizuri na kutoa fursa kujadili masuala yote yaliyoainishwa katika kikao cha baraza lililopita.
“kupitia baraza hili wajumbe tumekubali utekelezaji uliofanyika katika hoja za baraza lililopita na kupitisha rasimu ya bajeti mpya ya mwaka 2024/2025”, alisema Mndeme
Mndeme alisema wajumbe wa baraza wana imani mipango yote iliyopangwa kupitia baraza la wafanyakazi itaenda vizuri kwani hoja zilizopita zimeweza kufanyiwa kazi kwa asilimia 100 hivyo hata hoja zilizowasilishwa katika kikao cha baraza la nane zitafanyiwa kazi vizuri zaidi.
Comments
Post a Comment