JKCI yaweka kambi ya matibabu Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Dodoma
Afisa Utafiti wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima uwiano wa urefu
kwa uzito Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Juma Mkomi alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika Maonesho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini
Dodoma.
Daktari wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Daud Gwilenza akimsikiliza mwananchi aliyetembelea
banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Na JKCI
*******************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafikisha Kampeni ya
Jua Namba Zako kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kupitia maonesho
ya wiki ya utumishi wa umma yaliyoanza leo katika Viwanja vya Chinangali Park
vilivyopo jijini Dodoma.
Katika maonesho hayo wataalamu wa JKCI wanatoa elimu ya
umuhimu wa kupima na kufahamu shinikizo la juu la damu, mapigo ya moyo, wingi
wa sukari kwenye damu, uwiano wa uzito kwa urefu pamoja na wingi wa mafuta
kwenye damu.
Sambamba na elimu hiyo wananchi wanaotembelea katika banda la JKCI wanapata fursa ya kuyafahamu magonjwa ya moyo, namna ya kujikinga na magonjwa yaho lakini pia kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa kupimwa vipimo vya moyo, shinikizo la damu, sukari kwenye damu pamoja na uwiano wa urefu kwa uzito.
Comments
Post a Comment