Wananchi wahimizwa kutumia kampeni ya “Jua Namba Zako” kupima afya zao SABASABA

Mwenyekiti Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo akimsikiliza Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Afisa Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Oysterbay Suleiman Jafari akimuelezea namna shuka maalumu la Dozee linavyofanya kazi Mwenyekiti Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Daktari wa wagonjwa wa dharura wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospital ya Dar Group Peace Masaoe akimuelezea huduma za dharura zinazotolewa na Taasisi hiyo Mwenyekiti Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo alipotembelea banda la JKCI lililopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thabiti Ramadhani akimpatia zawadi Kamishna wa Tume ya madini Mhandishi Thenestina Mwasha alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thabiti Ramadhani akimpatia zawadi Kamishna wa Tume ya madini Dkt. Theresia Numbi alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Na JKCI

****************************************************************************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yapongezwa kufikisha kampeni ya Jua Namba Zako katika maonesho ya SABASABA kuiamasisha jamii kufanya uchunguzi wa viashiria vya magonjwa ya moyo kupitia maonesho hayo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janeth Reuben alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Dkt. Janeth alisema kampeni hiyo inatoa fursa kwa wananchi kutambua hali zao za afya mapema na kuchukua hatua za mapema dhidi ya magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyoambukiza.

“Nimefika katika banda la JKCI na nimejione kwa macho namna ambavyo huduma zinatolewa hapa, uwepo wa kampeni ya Jua Namba Zako katika maonesho haya ni fursa muhimu kwa jamii kupima na kutambua afya zao hivyo watumie vizuri maonesho haya kupima na kutambua namba zao”, alisema Dkt. Janeth.

Dkt. Janeth alisema sambamba na kampeni hiyo JKCI inatoa elimu kuhusu magonjwa ya moyo pamoja na kuwafanyia wananchi vipimo vikubwa vya moyo kwa urahisi bila hata kuvifuata hospitalini.

Aidha Dkt. Janeth amewaomba wananchi wanaotembelea maonesho hayo wasisite kufika katika banda la JKCI na kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa na Taasisi hiyo kupitia Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Heart Team Africa Foundation (HTAF) inayofanya jukumu hilo la kutafuta fedha za matibabu ya watoto.

“Gharama za matibabu ya moyo ni kubwa lakini watanzania tukiungana kwa pamoja tunaweza kukusanya fedha zitakazowasaidia watoto wenye magonjwa haya kupata huduma kwa urahisi na kwa wakati”, alisema Dkt. Janeth 

 

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi