Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI watembelea Hospitali ya JKCI Dar Group
Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Shamira Rwegoshora akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo huduma za matibabu zinazotolewa kwa wagonjwa wa dharura wakati wajumbe hao walipotembelea leo JKCI Dar Group iliyopo eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam. Mtaalamu wa tibaviungo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Jacqueline Mariki akifafanua jambo wakati wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Hospitali hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa. Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Rose Elibariki akiwaeleza huduma zinazotolewa katika wodi ya wazazi wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wajumbe hao walipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akijadilia...