Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya JKCI wapewa mafunzo ya kuwajengea uwezo zaidi wa kusimamia uendeshaji wa huduma
Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge
akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili yanayotolewa jijini Dar es
Salaam na Taasisi ya Uongozi kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi na mtoto Mkoa wa Rukwa Asha Izina akielezea namna ambavyo bodi hiyo imejipanga kuboresha huduma zinazotolewa na JKCI wakati wa mafunzo ya siku mbili yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. JKCI imeandaa mafunzo hayo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo zaidi wajumbe wa bodi ya Taasisi hiyo ili waweze kufanya kazi zao za uendeshaji wa bodi kwa ufanisi zaidi.
Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Adv. Haruni Matagane ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichangia
mada wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo zaidi wajumbe wa bodi
ya JKCI ili waweze kufanya kazi zao za uendeshaji kwa ufanisi zaidi
yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA.Godfrey Kilenga ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ,TAB Consult akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo zaidi wajumbe wa bodi ya JKCI ili waweze kufanya kazi zao za uendeshaji kwa ufanisi zaidi yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment