Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea cheti cha kuipa kibali JKCI kuwa Chuo cha kufundisha madaktari wa upasuaji wa moyo kupitia Chuo cha Madaktari wa upasuaji Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (COSECSA) kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo cha COSECSA Dkt. Kitugi Nungu jana Jijini Dar es Salaam
Daktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Bashiri Nyangasa akipokea cheti cha kumpa kibali kuwa mkufunzi wa kozi ya upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo cha Madaktari wa Upasuaji Afrika Mashariki, Kati na kusini mwa Afrika (COSECSA) Dkt. Kitugi Nungu jana Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha kumpa kibali kuwa mkufunzi wa kozi ya upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo Daktari bingwa wa Upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Evarist Nyawawa kilichotolewa na Chuo cha Madaktari wa Upasuaji Afrika Mashariki, Kati na kusini mwa Afrika (COSECSA) jana Jijini Dar es Salaam
Mhadhiri wa Chuo cha Madaktari wa Upasuaji Afrika Mashariki, Kati na kusini mwa Afrika (COSECSA) Dkt. Kitugi Nungu akimkabidhi cheti cha kumpa kibali kuwa mkufunzi wa kozi ya upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt. Alex Joseph wakati uongozi kutoka chuo hicho ulipowasilisha vyeti hivyo kwa wakufunzi wa JKCI jana jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Chuo cha Madaktari wa Upasuaji Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Africa (COSECSA) na madaktari wa JKCI waliotambuliwa na chuo hicho kuwa wakufunzi wa kozi ya upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo mara baada ya kukabidhiwa vyeti jana jijini Dar es Salaam
Picha na: JKCI
*****************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment