Dkt. Mollel atoa wito kwa wananchi kujitokeza kupima magonjwa ya moyo
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dkt. Maneno Mlawa akipokea tuzo kwa niaba ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel ya kutambua mchango wake wa kuanzishwa kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Beach jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI Prof. William Mahalu.
Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akitoa tuzo kwa Daktari bingwa wa moyo kutoka Chennai India Ulhas Pandurangi kwa ajili ya kumshukuru kwa kufundisha mfumo wa umeme wa moyo katika mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo uliofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Jumla ya washiriki 300 wanahudhuria mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akizungumza na washiriki wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa kwanza wa siku mbili wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Ledger Plaza, Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge na Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kwanza wa shambulio la moyo unaofanyika katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Godwin Mollel akifungua mkutano huo.
**********************************************************************************************************************************************************************************************************************
NAIBU Waziri wa Afya
Mhe. Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kupima ili
kufahamu hali zao za magonjwa ya moyo ili kutambua tatizo mapema na kuweza
kulizuia kabla ya madhara makubwa kutokea.
Mhe.Dkt. Mollel amesema
hayo leo Februari 17, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano wa
kwanza wa Shambulio la moyo uliohudhuriwa na Madaktari wa magonjwa ya moyo na
Wataalamu wengine wa masuala ya Afya nchini.
"Wito wangu ni
kwamba, suala la kupima moyo lisiwe mpaka usikie tatizo, iwe ni wakati wote,
ndio maana tunawataka Wataalamu watembee katika vituo mbalimbali vya Afya ili
kuhakikisha wanapima Watanzania wanaofika katika vituo ili wapate kujua hali
zao juu ya ugonjwa wa moyo”, alisema Mhe. Dkt. Mollel.
Sambamba na hilo Mhe.
Dkt. Mollel alitoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa
magonjwa hususan magonjwa ya moyo mara kwa mara ili kufanya utambuzi wa mapema
utaosaidia katika kutibu tatizo hilo.
Aidha Mhe. Dkt. Mollel
alisema Rais Samia amehidhinisha fedha nyingi sana katika uwekezaji kwenye
Sekta ya afya ili kununua vifaa tiba vya kisasa vinavyosaidia katika ufunguaji
wa kifua kwa kiasi kidogo sana na kutibu tatizo la moyo hali iliyosaidia
kupunguza muda wa mgonjwa kukaa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema dhumuni la
mkutano huo wa wataalamu wa masuala ya moyo ni kubadilishana uzoefu ili
kujiimarisha katika matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.
Alisema Duniani kote
zaidi ya watu milioni sita hupata tatizo la mshtuko wa ghafla wa moyo ambalo
linachangia vifo vingi kwa wananchi hivyo kuwataka kuchukuwa hatua mapema pindi
watakapohisi kuwa na tatizo hilo.
Mbali na hayo Dkt.
Kisenge alitoa wito kwa wananchi kuepuka kula vyakula vinavyoweza
kuchangia magonjwa ya mashambulio la moyo ikiwemo vyakula vya mafuta mengi, na
kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji pombe kupita kiasi na kufanya mazoezi
walau mara tatu kwa wiki kwa dakika 30.
Mkutano huo wa siku
mbilli wenye kauli mbiu isemayo shambulio la moyo ni hatari kwa maisha
yako, wahi Hospitali umehudhuriwa na washiriki 300 kutoka ndani na nje ya
nchi.
Comments
Post a Comment