HAKUNA MGONJWA ALIYEKUFA KWA KUKOSA PACEMAKER
Madaktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete
(JKCI) Tulizo Shemu na Yona Gandye wakimwekea mgonjwa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Pacemaker) leo tarehe 24/02/2023
**********************************************************************************************************************
Dar es
Salaam,
24/02/2022
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HAKUNA MGONJWA ALIYEKUFA KWA KUTOKUWEKEWA
“PACEMAKER”
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
inapenda kutoa ufafanuzi wa Habari iliyosambaa katika mitandaoni ya kijamii
kuwa “Huduma ya Pace Maker haipo Muhimbili, Wagonjwa wanakufa” taarifa
hiyo siyo ya kweli na ipuuzwe, kwani hakuna mgonjwa aliyekufa kutokana na
tatizo la kutokuwekewa kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri “Pacemaker”.
Taasisi ilikuwa na upungufu wa Pacemaker
kwa muda wa wiki mbili ilitokana na mtoa huduma ya kusambaza vifaa hivyo
kuchelewa kuvileta hapa nchini kutoka nchini Uholanzi. Hata hivyo, iwapo
inatokea upungufu wa vifaa hivi Taasisi inautaratibu wa kuhifadhi vichache kwa
ajili ya kutumika kwa wagonjwa wa dharura kwani wagonjwa wanaowekewa Pacemaker
wako wa aina mbili kuna wa dharura na wale wanaoweza kusubiri.
Kutokana na changamoto hii wagonjwa
wote waliokuwa wa dharura waliwekewa Pacemaker ambapo kwa wiki ya tarehe
06-12/2/2023 wagonjwa watatu waliwekewa kifaa hicho. Wiki ya tarehe
13-19/02/2023 hakukuwa na mgonjwa wa dharura aliyehitaji kuwekewa Pacemaker.
Siku ya jana tarehe 23/2/2023 Taasisi
ilipokea Pacemaker kutoka kwa mtoa huduma ya kusambaza vifaa hivyo na siku ya
jana wagonjwa watatu waliwekewa kifaa hicho na leo tarehe 24/02/2023 wagonjwa
watano wanawekewa pia wanaohitaji kuwekewa Pacemaker wamepewa taarifa kufika
Hospitali.
Aidha, endapo itatokea Taasisi
ikaishiwa kabisa Pacemaker ingawa haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwake mwaka
2015, kuna utaratibu ambao umewekwa wa kuazima vifaa hivyo kutoka Hospitali za
hapa nchini na Afrika ya Mashariki ambazo zinatoa huduma ya upasuaji wa moyo.
Taasisi inatoa onyo kwa watu waliotoa
taarifa hii ya uongo ambayo imezua sintofahamu kwa wananchi pamoja na wagonjwa
wetu kuacha mara moja kufanya hivyo. Tunaendelea kusisitiza iwapo mtu anahitaji
kupata ufafanuzi kuhusu huduma zetu au anakutana na changamoto yoyote ile ya
kimatibabu afike katika Taasisi yetu au apige
simu namba +255688027982 au +255782042019 kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi.
“Afya ya Moyo
Wako ni Jukumu Letu”.
Imetolewa na :
Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano - JKCI
Comments
Post a Comment