Kanisa la Christ Mandate lasambaza upendo kwa watoto wenye magonjwa ya moyo
Katibu wa kanisa la Christ Mandate Elizabeth Lema akicheza na mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wakati waumini wa kanisa hilo walipopeleka mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na mchungaji wa kanisa hilo kwa watoto hao wakiwa na lengo la kusambaza upendo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam
Waumini kutoka Kanisa la Christ Mandate Elizabeth Lema na Aluseta Kansary wakiwakabidhi wazazi wa watoto waliolazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na mchungaji wa kanisa hilo wakiwa na lengo la kusambaza upendo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam
Muumini kutoka kanisa la Christ Mandate Nuru Shimbi akimkabidhi mama wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Warda Mgeruka mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na mchungaji wa kanisa hilo wakiwa na lengo la kusambaza upendo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa wodi ya watoto wenye magonjwa ya Moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Grace Sanga akipokea bahasha ya fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya watoto 10 wanaotibiwa katika Taasisi hiyo zilizotolewa na Mchungaji wa Kanisa la Christ Mandate na kuwasilishwa na katibu wa kanisa hilo Elizabeth Lema wakati waumini wa kanisa hilo walipowatembela watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali wakiwa na lengo la kusambaza upendo kwa watoto hao leo Jijini Dar es Salaam
Katibu wa kanisa la Christ Mandate Elizabeth Lema akimkabidhi mama wa mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Joyce Yona mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na mchungaji wa kanisa hilo wakiwa na lengo la kusambaza upendo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam
Picha na: JKCI
****************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment