Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI watembelea Hospitali ya JKCI Dar Group
Daktari bingwa wa magonjwa ya dharura wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Shamira Rwegoshora akiwaelezea wajumbe wa Bodi
ya Wadhamini ya Taasisi hiyo huduma za matibabu zinazotolewa kwa wagonjwa wa
dharura wakati wajumbe hao walipotembelea leo JKCI Dar Group iliyopo eneo la TAZARA
jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa tibaviungo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dar Group Jacqueline Mariki akifafanua jambo wakati wajumbe wa Bodi ya Wadhamini
ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Hospitali hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma
zinazotolewa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akijadiliana na viongozi wa Taasisi hiyo namna
ya kuboresha huduma za matibabu katika hospitali ya JKCI Dar Group wakati
wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea Hospitali hiyo leo kwa ajili ya kuona
huduma za matibabu zinazotolewa.
Comments
Post a Comment