Idara zilizotoa huduma bora kwa wateja zapongezwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akikabidhi cheti cha mshindi wa kwanza katika kutoa huduma bora kwa wateja kiongozi wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) Afisa Muuguzi Lucia Kabeya wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kupitia taarifa ya ukaguzi wa ndani wa huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kitengo cha ICU kimeongoza kwa kutoa huduma bora kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha mshindi wa pili katika kutoa huduma
bora kwa wateja Mkuu wa Idara ya Famasia Wellu Kaali wakati wa kikao cha
wafanyakazi wa Taasisi hiyo kupitia taarifa ya ukaguzi wa ndani wa huduma zinazotolewa
na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Idara ya Famasia imekuwa ya pili
katika kutoa huduma bora kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akikabidhi cheti cha mshindi wa tatu katika kutoa huduma
bora kwa wateja mwakilishi kutoka Maabara Emanuel Mgao wakati wa kikao cha
wafanyakazi wa Taasisi hiyo kupitia taarifa ya ukaguzi wa ndani wa huduma
zinazotolewa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Idara ya Maabara
imekuwa ya tatu katika kutoa huduma bora kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi
Desemba 2022
Mkuu wa Kitengo cha Huduma Bora kwa Wateja kutoka Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Naiz Majani akielezea namna ambavyo kitengo
hicho kimefanya ukaguzi wa ndani wa huduma zinazotolewa kwa mwezi Oktoba hadi
Desemba wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika jana
katika ukumbi wa JKCI uliopo jijini Dar es Salaam.
Picha na: JKCI
******************************************************************************************************
Comments
Post a Comment