Watu 29,000 wachunguzwa magonjwa mbalimbali kambi ya madaktari bingwa mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Mkombachepa wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya siku nane ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya siku nane ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Afisa kumbukumbu na taarifa za afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akigawa vipeperushi vya shinikizo la juu la damu na lishe kwa wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kutibiwa moyo wakati...