Watu 29,000 wachunguzwa magonjwa mbalimbali kambi ya madaktari bingwa mkoani Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Charles Mkombachepa wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya siku nane ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya siku nane ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Afisa kumbukumbu na taarifa za afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Saad Kamtoi akigawa vipeperushi vya shinikizo la juu la damu na lishe kwa wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kutibiwa moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima shinikizo la damu mwananchi wa mkoa wa Arusha aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kutibiwa moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma ya matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

************************************************************************************************************************************************************************************************************
Jumla ya watu 29,000 wamechunguzwa magonjwa mbalimbali katika kambi maalumu ya madaktari bingwa inayofanyika katika viwanja vya Sheik Amri Abed vilivyopo mkoani Arusha. 

Wagonjwa waliochunguzwa kwa upande wa magonjwa ya moyo ni 1,534 watu wazima wakiwa 1,379 na watoto 155 wagonjwa 187 wanapelekwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupatiwa matibabu ya kibingwa ambapo  gharama zote za matibabu hayo  zinalipwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 Akizugumza kuhusu kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge alisema zoezi la upimaji na matibabu limeenda vizuri ambapo wananchi wamepata fursa  ya kuhudumiwa magonjwa mbalimbali na madaktari bingwa waliobobea  katika magonjwa ya binadamu. 

Dkt. Kisenge wagonjwa 187 wamekutwa na matatizo mbalimbali ya moyo katika hao watoto 53 wanatakiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo hii ni kutokana  na valve zao pamoja na mishipa ya damu ya moyo kupata matatizo .

 "Watoto hao wote matibabu yao yatagharamiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja inagharimu kiasi cha shs.12 milioni na hivyo wananchi mnapaswa kuona ni jambo la kishujaa sana lililofanywa na Rais wetu kwani kwa kawaida mwananchi wa kawaida ni ngumu sana kumudu hizo gharama hizo”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktarin bingwa wa moyo alisema muda wa matibabu  hayo  umeongzwa  hadi siku ya kesho kwaajili ya kumaliza wagonjwa ambao wanaendelea kupata huduma katika kambi hiyo ili waweze kupata huduma wanayostahili.

 "Takwimu zinaonyesha duniani kote kuwa asilimia kubwa ya watu wanaopoteza maisha wanatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo hivyo elimu zaidi inahitajika kutolewa kwaajili ya wananchi kufuata mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi mara  kwa mara, kutovuta sigara, kunywa pombe kwa kiasi sambamba na kupunguza vyakula vya wanga na kuzingatia lishe bora”, alisema Dkt. Kisenge.

 Hata hivyo Dkt. Kisenge alisema Taasisi hiyo ina mpango mkakati wa kufungua kitengo cha Moyo mkoani Arusha  mwezi wa tisa kwaajili ya kurahisisha utoaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa Arusha na kuondokana na gharama ya kuifuata huduma hiyo jijini Dar es  Salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda alishukuru kwa namna ambavyo huduma hiyo inavyotolewa na madaktari bingwa kwani mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa sana .

"Haya yote yanayofanyika hapa ni upendo wa Mhe. Rais Dkt. Samia kwa wananchi wake kwa kupunguza gharama ya kufuata huduma  hiyo jijini Dar.es Salaam kwani kwa kufanya hivyo ni faraja kubwa sana kitendo cha kuona matatizo ya watu sio jambo la kawaida ,tumuombee sana Rais Samia wetu kwani anapambana kutatua changamoto za wananchi kwa kiwango kikubwa sana”,alisema Mhe. Makonda.

Nao wananchi waliohudumiwa katika banda hilo la JKCI walishukuru kwa huduma waliyoipata na kusema kuwa imewapunguzia gharama za kufua huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa namna ambavyo  amewezesha uwepo wa kambi hii ambapo mume wangu amepimwa   na  kugundulika  mishipa  yake ya damu ya moyo imetanuka na kuweza kupatiwa dawa kwani anaishi maisha ya shida na ingekuwa ngumu sana kupata matibabu kutokana na gharama hiyo”,alishukuru Tabu Juma.

“Nimepimwa moyo wangu na kukutwa na tatizo la umeme wa moyo na kukutwa na tatizo la umeme wa moyo, nimepewa dawa za kutumia pamoja na rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI. Ninashukuru kwa huduma niliyoipata kwani katika hali ya kawaida ingenichukuwa muda mrefu kupata huduma hii”, alisema Musa Massawe.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari