Askofu Dkt. Mollel awajulia hali wananchi wanaopata huduma ya matibabu ya moyo

Askofu wa Kanisa la Kiinjilisti la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Abel Mollel akiwapa pole wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda akimpa pole mwananchi wa mkoa huo aliyefika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi  na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kulia ni Askofu wa Kanisa la Kiinjilisti la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Abel Mollel.

Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akichukuwa fomu za matibabu za wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika  katika banda la taasisi hiyo  kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi  na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Wananchi  wa mkoa wa Arusha waliofika  katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisubiri kupata huduma za uchunguzi  na matibabu ya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari