Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel atembelea kambi ya uchunguzi na matibabu inayofanyika mkoani Arusha

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda mara baada ya kupokea mchango wa dawa kutoka kwa wadau wa afya ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akisalimiana na viongozi wa dini waliofika katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwashukuru wataalamu wa afya wanaotoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwajulia hali wananchi waliofika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kushoto ni Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt.Godwin Mollel akisalimiana na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanaotoa huduma za matibabu ya moyo kwa  wananchi wa mkoa wa Arusha waliofika  katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wakazi wa Arusha waliokuwa wanasubiri kuchukuwa dawa baada ya kupimwa na kugundulika kuwa na magonjwa mbalimbali katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Kulia  ni Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.


Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wakazi wa Arusha waliokuwa wanasubiri kuchukuwa miwani baada ya kupimwa na kukutwa na matatizo ya macho katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari