Wakazi wa Ilala watibiwa moyo bila malipo

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edwald Mpogolo akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa Dar es Salaam leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo ambapo kampeni hiyo afya check ni mwendelezo  wa siku 10 inayofanyika katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Gloriamaria Kunambi akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mtoto aliyefika katika kampeni ya afya check inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo ni mwendelezo wa upimaji wa siku 10 unaofanyika katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Agnes Ndangamila akimshauri mwananchi aliyetembelea banda la JKCI wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa afya bila malipo kwa wakazi wa Dar es Salaam leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo ambapo kampeni hiyo ni mwendelezo wa siku 10 katika Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha na: Hamis Mussa

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari