Viongozi wa Serikali ya Nigeria watembelea JKCI
Mkurugenzi wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akiwaeleza huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo
viongozi wa Serikali ya Nigeria waliotembelea taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili ya kuona
huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji
uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini.
Viongozi wa Serikali ya Nigeria wakiangalia video
inayoonyesha huduma za kibingwa za matibabu ya moyo zinazotolewa katika Taasisi
ya Moyo Jakaya Kiwete (JKCI) walipotembelea taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili
ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji
uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini
Viongozi kutoka Serikali ya Nigeria na wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara yao ya kutembelea taasisi hiyo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya kibingwa ya moyo nchini.
Na: JKCI
***********************************************************************************************************************
Viongozi wa Serikali ya Nigeria wametembelea Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa
pamoja na kuangalia uwekezaji uliofanywa na Serikali katika matibabu ya
kibingwa ya moyo nchini.
Ziara hiyo imefanyika hivi karibuni katika Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam baada ya viongozi hao kuwasili nchini kwaajili ya
kuhuduria mkutano wa kujadili masuala ya ulinzi na usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge alisema baada ya viongozi hao kupata taarifa za huduma
zinazotolewa JKCI waliweza kutumia fursa waliyoipata kufika JKCI na kujionea
wenyewe huduma zilizopo.
“Ugeni wa viongozi wa serikali kutoka nchini Nigeria umetembelea
maeneo mbalimbali ya taasisi yetu na kuangalia jinsi gani huduma za tiba ya
moyo zinatolewa, ambapo tumewapitisha katika vyumba vya upasuaji wa moyo pamoja
na kutembelea kliniki maalumu ya VIP”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge alisema viongozi hao wamefurahishwa na huduma
zinazotolewa katika taasisi hiyo na kuahidi watakaporejea nchini mwao wataenda
kuwa mabalozi wa kuwajulisha wagonjwa wa moyo kufika JKCI kwaajili ya matibabu.
“Baada ya kutembelea taasisi yetu wapo baadhi tumewapatia
huduma na kuwafanyia uchunguzi wa magonjwa ya moyo na kuridhika na huduma zetu
zinazotolewa katika kliniki maalumu ya VIP”, alisema Dkt. Kisenge.
Comments
Post a Comment