JKCI yapata tuzo katika kongamano la kisayansi nchini Kenya

Tafiti mbili kati ya tano za magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimechaguliwa kuwa tafiti bora na kupewa tuzo katika kongamano la kisayansi la 41 la mabingwa wa moyo nchini Kenya. Tafiti hizo mbili zilizopewa tuzo zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy) utafiti ambao umechukua miaka nane kufuatilia tatizo hilo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo alisema aliwasilisha tafiti hizo katika kongamano la kisayansi la 41 lililoandaliwa na chama cha madaktari bingwa wa moyo wa Kenya (Kenya Cardiac Society) na kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. “Tafiti mbili kutoka JKCI zilichaguliwa kuingia kwenye ushindani wa tafiti bora na kupewa tuzo, tafiti hizi zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy)”, alisema Dkt. Pedro Dkt. Pedro ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunz...