Viongozi mbalimbali wapongeza huduma zinazotolewa na JKCI katika banda la Sabasaba

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samwel George akimueleza Waziri wa afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui namna daktari aliyepo JKCI anaweza kusoma majibu ya mgonjwa anayetibiwa kwa kifaa maalumu kijulikanacho kwa jina la DOZEE kinachotumika kufuatilia maendeleo ya mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani alipotembelea banda la JKCI lililopo katika maonesho ya Sabasaba.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eben Ngowi akimpima urefu na uzito Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Awadhi Juma Haji alipotembelea banda taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh akimsikiliza Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildegard Karau alipokuwa akimwelezea kuhusu huduma zinazotolewa katika banda la taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Nicole Kinyawa akimpima shinikizo la damu Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa maonesho ya sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam

Afisa Takwimu na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akifanya mahojiano na raia wa Iran Monirch Sabagh aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Elius Birago akizungumza na raia wa Ujerumani aliyetembelea banda la taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 Na: JKCI

*******************************************************************************************************************

Viongozi mbalimbali wa Serikali wamepongeza huduma za matibabu na elimu ya lishe zinazotolewa katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam.

Pongezi hizo zimetolewa leo wakati viongozi hao walipotembelea banda la JKCI na kusema JKCI imeonyesha mabadiliko makubwa katika kutoa huduma kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Akizungumza alipotembelea banda hilo Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui alisema JKCI kutumia huduma ya afya mtandao kuweka miadi ya kuonana na daktari ni moja ya teknolojia ya kisasa inayomsaidia mgonjwa kupata huduma za afya kwa wakati.

“Matumizi ya teknolojia katika Taasisi hii yanatumika vizuri sana kwani mfumo wa huduma za afya mtandao unaotumika kwa wananchi kukutana na wataalamu wa JKCI kupitia mtandao unatuwezesha kuzungumza na daktari tukiwa mahali popote duniani”, alisema Mhe. Mazrui

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Awadhi Juma Haji aliwapongeza wataalamu wa JKCI kwa kutoa huduma kwa wananchi katika maonesho ya Sabasaba.

Kamishna Haji alisema wananchi wanaposogezewa huduma karibu uwapa nafasi kutumia muda huo kupima afya tofauti na kama wangeambiwa waifuate huduma hiyo mahali zilipo hospitali.

“Nimetembelea banda hili na kupata elimu nzuri sana kuhusu magonjwa ya moyo, wananchi wanaopenda kupata elimu sahihi kuhusu magonjwa haya wasisite kutembelea banda la JKCI”, alisema Kamishina Haji

Naye Naibu Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh aliupongeza uongozi wa JKCI kwa kuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo nchini.

Mhe. Hafidh alisema kutoa huduma za moyo katika maonesho ya Sabasaba kunawapa fursa wananchi wengi kupima afya zao kwani maonesho hayo yanatembelewa na wananchi wengi.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari