JKCI yapata tuzo katika kongamano la kisayansi nchini Kenya

 

Tafiti mbili kati ya tano za magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimechaguliwa kuwa tafiti bora na kupewa tuzo katika kongamano la kisayansi la 41 la mabingwa wa moyo nchini Kenya.

Tafiti hizo mbili zilizopewa tuzo zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy) utafiti ambao umechukua miaka nane kufuatilia tatizo hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo alisema aliwasilisha tafiti hizo katika kongamano la kisayansi la 41 lililoandaliwa na chama cha madaktari bingwa wa moyo wa Kenya (Kenya Cardiac Society) na kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Tafiti mbili kutoka JKCI zilichaguliwa kuingia kwenye ushindani wa tafiti bora na kupewa tuzo, tafiti hizi zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy)”, alisema Dkt. Pedro

Dkt. Pedro ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo alisema Kongamano hilo lilikuwa na jumla ya tafiti 40 zilizowasilishwa ambapo tafiti 8 zilichaguliwa kuwa tafiti bora na kustahili kupewa tuzo.

“Mbali na tafiti mbili za JKCI kupewa tuzo mimi kama mwandishi wa tafiti hizo  nimekaribishwa katika mkutano kama huu wa mwakani na gharama zote zitalipiwa na waandaaji wa mkutano huo”, alisema Dkt. Pedro.


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini