Rais mstaafu Mhe. Dkt. Kikwete atembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete katika maonesho ya sabasaba
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mahawa Asenga akimweleza kuhusu huduma ya upimaji wa shinikizo la damu na kiwango cha sukari kwenye damu anayoitoa kwa wananchi wanaotembelea banda hilo lililopo katika maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanaoshiriki katika maonesho ya sabasaba alipotembelea banda la taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Modesta Nyagawa akiwafundisha wananchi waliotembelea banda la taasisi hiyo namna ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi wakati wa maonesho ya sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha na Hamisi Mussa
Comments
Post a Comment