Wananchi wa Wilaya ya Ilala wajitokeza kupima moyo
Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Mahamoud Hassan akimpima wingi wa sukari kwenye damu
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la
Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya
Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali
ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Hospitali ya Dar Group Sabina Zakaria akimpima shinikizo la damu Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Said Sidde wakati wa ufunguzi wa
kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika
Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya
siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya
Mbunge wa jimbo la Ilala.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu pamoja na Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Said Sidde wakikata utepe kuashiria
uzinduzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba
inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group
kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wananchi wa Ilala wakati wa uzinduzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akielezea huduma zitakatotolewa wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu
Wananchi wa Wilaya ya Ilala wakiendelea na huduma za vipimo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika kwa siku nne katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu
Na: Stella Gama
********************************************************************************************************************
Wananchi wa Wilaya ya Ilala wametakiwa kujitokeza kwa wingi kufanya
uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika kambi maalumu ijulikanayo kwa jina la Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba.
Kambi hiyo maalumu iliyoanza leo inafanyika kwa siku nne
katika Zahanati ya Bungoni iliyopo Kata ya Ilala kwa kutoa huduma bila gharama
kwa wananchi wote watakaofika kwaajili ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo,
sukari, na shinikizo la damu.
Akizungumzia wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa
Azzan Zungu alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kurahisisha huduma za matibabu na kuwafuata wananchi mahali
walipo.
“Nawapongeza wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kufanikisha huduma hii ya upimaji kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala,
Matibabu ya moyo yana gharama kubwa lakini JKCI imetuletea hapa vifaa vya
kisasa na mabingwa wa moyo ili waweze kutufanyia uchunguzi na kutupa ushauri,
tutumie fursa hii kupima afya zetu”, alisema Mhe. Zungu
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya JKCI Dar Group Dkt.
Tulizo Shemu alisema JKCI imekuwa ikisogeza huduma za uchunguzi wa magonjwa ya
moyo kwa wananchi kuwapa fursa kupima afya zao kwani watu wengi hawana tabia ya
kupima afya zao mara kwa mara.
“Tumekuwa tukipima afya zetu pale tunapoona changamoto za
kiafya katika miili yetu lakini hatuna tabia ya kufanya uchunguzi kabla ya
kuumwa ndio maana JKCI tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali kufikisha
huduma za uchunguzi katika jamii kuijengea jamii yetu kuwa na tabia ya
kuchunguza afya zetu mara kwa mara”, alisema Dkt. Shemu
Dkt. Shemu alimshukuru Mbunge wa Jimbo la Ilala kwa
kuwakumbuka wananchi wa Ilala na kuwafikishia huduma hizo za kibingwa kwani
kati yao wapo ambao wasingeweza kuzifuata mahali zilipo.
“Tunaishukuru sana ofisi ya Mbunge wa Ilala pamoja na wadau
wengine kwa kuweza kushirikiana kwa pamoja kufanikisha huduma hii leo hapa
Ilala, pia tunawashukuru wadau wetu kampuni za dawa ambao mmekuwa mkishirikiana
nasi katika kambi zetu na kuwapatia wananchi dawa bila gharama”, alisema Dkt.
Shemu
Naye mwananchi aliyejitokeza kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi
wa afya Thabia Mohamed alisema huduma za uchunguzi wa afya kupitia kambi hiyo zimewasaidia
wananchi kuepuka gharama za matibabu kama wangezifuta hospitali.
Thabia aliomba huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo
ziendelee kutolewa kwa karibu kwa wananchi ili ziweze kuwawezesha kupima afya
zao na kuweza kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo.
“Baada ya kupata taarifa ya kambi hii ya matibabu wananchi wa
Ilala tulikuwa na shahuku kubwa hatimaye leo imefika na tupo hapa toka asubuhi
tunaendelea na huduma za vipimo vya moyo lakini pia tumepata elimu kuhusu
magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo”, alisema Thabia
Comments
Post a Comment